Pages

Pages

Thursday, February 10, 2011

MGAO WA UMEME:TANESCO KUENDELEZA MATESO

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu hali halisi ya mgao wa umeme unaoendelea nchini, ambao unasababishwa na kuzidi kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa la Mtera ambapo hupungua sentimita tatu kila siku. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Badra Masoud.

Mashambulio yazuka Sudan Kusini

Maafisa wanasema watu wasiopungua 16 wameuawa baada ya waasi kushambulia jeshi la Sudan Kusini, na kuteteresha makubaliano ya kusitisha mapigano.
Sudan
Harakati wakati wa upigaji kura
Wapiganaji wanaomtii Goerge Athor wamelipua magari mawili ya kijeshi karibu na mji wa Fangak, katika jimbo la Jonglei, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la kusini.

Saini

Bw Athor aliamua kubeba silaha mwaka jana, kwa madai kuwa kulikuwa na wizi katika uchaguzi wa jimbo, lakini alitia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi uliopita.
Mapigano haya yanakuja wakati Sudan Kusini inajiandaa kutengana na upande wa Kaskazini.

Waasi 12

Asilimia 99 ya watu wa kusini walipiga kura ya kutaka kujitenga, katika kura ya maoni ya mwezi uliopita, kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa wiki hii.
Msemaji wa jeshi la upande wa kusini Philip Aguer amesema wanajeshi wanne na waasi 12 wameuawa, lakini anahofia watu zaidi wamekufa.

kuchochea

"Tunasubiri taarifa kamili za waliopoteza maisha," amesema.
Wakati Bw Athor akiamua kuchukua silala, upande wa kusini ulimtuhumu kwa kutumiwa na upande wa kaskazini ili kuchochea ghasia na kuharibu kura ya maoni, tuhuma ambazo maafisa wa upande wa kaskazini unazikana.




MISS UTALII 2011 MATAMBO YAANZA

                             Hapa wakiwa katika hifadhi ya tarangire
                                    Washiriki wa utalii wakicheza kutafuta miss utalii tarangire
                             Baadhi ya washiriki wa miss utalii wakiwa wamepunzika katika hifadhi ya Tarangire
                              Hapa wakiwa katika maporomoko ya mlima udizungwa

Waziri wa Sudan Kusini auawa

Waziri mmoja kutoka serikali ya Sudan kusini ameuawa ndani ya jengo la wizara yake mjini Juba.
Philip Aguer wa jeshi la SPLM alisema, waziri wa maendeleo ya ushirika na masuala ya vijijini Jimmy Lemi Milla ameuliwa na aliyekuwa mfanyakazi wake .
Mtu huyo naye alimwuua mlinzi wa waziri huyo ambapo baadae kukamatwa.

Waziri wa Sudan Kusini Jimmy Lemi Milla
Tukio hilo linatokea siku chache tu baada ya matokeo ya kura za maoni kuthibitishwa kuwa Sudan Kusini itakuwa taifa jipya duniani ambapo litaidhinishwa rasmi Julai 9.
Takriban asilimia 99 ya raia wa Sudan kusini walipiga kura ya kujitenga katika kura za maoni zilizofanyika mwezi uliopita.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir alisema atakubali matokeo.
Maafisa wa chama tawala cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM) wanaamini lengo la uyfatuliaji risasi uliotokea siku ya Jumatano ni la kibinafsi zaidi kuliko kisiasa.
Lakini mwandishi wa BBC Peter Martell wa Juba amesema ni wazi kuwa kuna changamoto za kiusalama wakati Sudan kusini inapoelekea kupata uhuru wake rasmi.


HARAKATI ZA HATMA YA KUMJUA MMLIKI WA DOWANS FEB 24
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Februari 24 mwaka huu itaanza rasmi kusikiliza kesi ya tuhuma za kughushi na kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa serikali inayomkabili Naeem Adam Gile.
Wakili wa serikali, Shadrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, alieleza kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upande wa Jamhuri upo tayari kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Lema alisema anakubaliana na ombi hilo na anaiahirisha kesi hiyo hadi Februari 24 mwaka huu ambapo itakuja kwa ajili ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao.
Janurai 13 mwaka 2009, ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili Mkuu wa Serikali, Stanslaus Boniface kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashitaka matano ambayo aliyatenda kwa nyakati tofauti.
Alidai kuwa Machi 13, 2006, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa akiwa na dhamira ya kutenda kosa, alighushi hati ya nguvu ya kisheria (power of attorney) inayoonyesha imetolewa na Hamed Gile, ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, kwamba amemruhusu kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini.
Alisema shitaka la pili ni kutoa taarifa za uongo ambapo alieleza kuwa Machi 20 mwaka 2006, katika eneo la Ubungo, Umeme Park, Barabara ya Morogoro, mshitakiwa alitoa hati hiyo ya nguvu ya kisheria inayomuidhinisha yeye kwamba ameruhusiwa kufanya kazi ya kampuni hiyo ya Marekani hapa nchini.
Aliendelea kudai kuwa, shitaka la tatu linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma na kwamba Julai 20, 2004 eneo la Ubungo Umeme Park, alitoa taarifa ya uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme (TANESCO). Kwamba Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100 kwa Tanzania ili wajumbe wa bodi hiyo waweze kumpendekeza kupewa tenda ya kutoa huduma hiyo.
Katika shitaka la nne, alidai Juni, 2006 jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme kwa kiwango hicho ili apewe tenda hiyo.
Aidha, alidai katika shitaka la tano mshtakiwa akifahamu na kwa ulaghai, alitoa hati ya nguvu ya kisheria iliyotolewa Machi 3, mwaka 2006 iliyokuwa ikimuonyesha kuwa ameruhusiwa na Mwenyekiti wa Kampuni, Hemed Gile, kufanya kazi za kampuni hiyo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment