Pages

Pages

Saturday, February 19, 2011

RAIS MUSEVENI AELEKEA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU

 Matokeo yasiyokuwa rasmi ya kura ya urais nchini Uganda yanaonyesha kuwa rais aliyepo madarakani Yoweri Museveni,yuko katika nafasi nzuri ya kunyakuwa ushindi kulitawala tena taifa hilo kwa mhula wa nne.


Bwana Museveni amekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka ishirni na tano.
Wachunguzi wa uchaguzi huo kutoka umoja wa ulaya wameutaja kuwa wa amani lakini msemaji wa upinzani unaoongozwa na Kisa Besigye amesema kumekuwa na visa vya wapiga kura kutishiwa.

Rais Museveni akiwa kwenye foleni akisubiri kupiga kura
Mwandishi wa BBC kuhusu maswala ya Afrika mashariki anasema kiasi kikubwa cha pesa za serikali kimetumiwa kuwashawishi wapiga kura kumchaguwa tena rais museveni.


TUNDU LISSU AMNYIMA USINGIZI ANNA MAKINDA 
   Tundu lissu akikamua vifungu vya kanuni bungeni.
  Mbunge kutoka singida Tundu Lissu amekuwa changamoto kubwa kwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Anna Makinda kwa kumbana na vifungu vya kanuni ambapo anapoonekana kugandamiza wapinzani bungeni.
  Hata bi. makinda amekili kuwa changamoto hizo zimemjenga sana kwani wabunge wote wapo kwaajili ya maslai ya taifa na sio uchama,bunge limesitishwa kwa muda lakini hapo jana wabunge wamejitolea posho yao ya siku ya jana kwaajili ya kusaidia wahanga wa mabomu ya gongo la mboto.


     KESI YA MATUMIZI MABAYA YA OFISI ZA UMMA HII HAPA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, inaendelea kufanya jitihada za kukamilisha uchapaji wa mwenendo wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma inayomkabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, na wenzake licha ya kukabiliwa na tatizo la mgawo wa umeme na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.
Hakimu Mkazi Mustapher Siyani aliyasema hayo jana wakati kesi ilipokuja jana kwaajili ya kutajwa na kuangalia kama tayari uongozi wa mahakama umeishachapa mwenendo wa kesi hiyo ili mahakama ipange tarehe ya mawakili wa upande wa utetezi kuwasilisha hoja za wateja wao kama wana kesi ya kujibu au la.
“Mwenendo wa kesi hii, hivi karibuni upande wa Jamhuri ulifunga kesi yao na mahakama hii ikatoa amri ya upande wa utetezi kupatia mwenendo huo….ni kiri kwamba bado mahakama haijamaliza kuchapa mwenendo huo ila nawaakikishia mahakama hii inafanya jitihada kuhakikisha mwenendo huo unachapwa licha ya kuwepo kwa mgao wa umeme.
“Kwa sababu hiyo basi naairisha kesi hii hadi Machi 18 mwaka huu, kesi itakuja kwaajili ya kutajwa pamoja na kuangalia kama tayari mwenendo huo kama utakuwa tayari umeishaandaliwa,” alisema Hakimu Siyani.
Januari 20, mwaka huu, Wakili Mkuu wa Serikali Stanslaus Boniface aliiambia mahakama kuwa upande wa Jamhuri umefunga rasmi kesi yao. Mbali na Mramba washtakiwa wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Gray Mgonja.

No comments:

Post a Comment