Pages

Pages

Thursday, March 3, 2011

MAHAKAMA NA MKATABA WA DOWANS

 MODEL OF A DAY


MAHAKAMA vs DOWANS
 Ile Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuingia mkataba mpya na Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikiwa ni hatua za muda mfupi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Hata hivyo, Mahakama Kuu imeizuia Serikali na Tanesco kuchukua hatua yoyote inayohusiana na mazungumzo au mkataba wa aina yoyote baina yake na Dowans bila ridhaa yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba alisema: "Kamati imependekeza mambo 30 ikiwamo kuwashwa kwa mitambo ya Dowans haraka na serikali itoe fedha zaidi kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL. Hatua hii imefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.''

Makamba alisema pia kwamba kamati imependekeza kupunguzwa kwa megawati 50 kutoka katika migodi ya madini inayotumia umeme wa megawati 125 ili zipelekwe kwa wananchi.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga alisema mapendekezo hayo watayakabidhi katika Ofisi za Bunge na kwamba yatatangzwa na Spika, Anne Makinda

 

Mahakama yachunguza 'uhalifu'wa Gaddafi


Brega
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu amesema atamchunguza kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, watoto wake wa kiume na viongozi waandamizi kwa uhalifu dhidi ya binadamu.
Luis Moreno-Ocampo alisema hakuna mwenye haki ya kuwaua raia.
Maelfu ya watu wanadhaniwa kufariki dunia katika ghasia baada majeshi ya usalama kuwalenga waandamanaji katika vurugu zilizoanza Februari 17.
Kanali Gaddafi aliahidi kuendelea kupambana licha ya kukosa udhibiti wa eneo kubwa la nchi hiyo.
Vyanzo vya habari mjini Brega vilisema, mapema siku ya Jumatano majeshi yake yalishambulia kwa kutumia ndege katika mji huo wenye mafuta.
Mashambulio hayo yalifanyika siku moja baada ya kuwepo mapigano baina ya waasi na majeshi ya serikali katika mji ambapo watu 14 walifariki dunia.
Alisema, " Ofisi ya mwendesha mashtaka aliamua kufanya uchunguzi kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyofanywa Libya tangu Februari 15."
" Ujumbe wa waandamanaji waliofanya kwa amani walishambuliwa na majeshi ya usalama.
" Katika wiki zijazo ofisi hii itachunguza ni wepi wanahusika zaidi katika mashambulio mazito zaidi, na kwa uhalifu mbaya zaidi uliofanywa Libya."
Lakini mwendesha mashtaka huyo pia alisema upinzani nao utachunguzwa kama ulifanya uhalifu wowote.


NIVEA NEW PRODUCT


What you see: An anti-wrinkle care system that includes a light cream and a moisturizing night cream which increases the skin’s natural Q10 level to fight wrinkles from within. The system also promises additional benefits, namely safeguarding your skin against sun damage by offering UVA and UVB protection.

What you get: The day cream is a non-greasy formula that works well for combination to oily skin and the intensely hydrating night cream works by replenishing the skin’s moisture levels. An optimized UVA filter protects the skin against ageing and prevents new wrinkles from forming.

What to expect: The lightly-scented, cream goes on smoothly and is absorbed well into the skin. Just like one would expect from Nivea, the creams have immediate moisturizing effects that you can witness from day one. Expect to notice some difference after two weeks of regular use and at the end of five weeks, expect to see a significant reduction in fine lines.

..THE GREAT AINGIA NA .''''THE SHOCK''


Kama alivyojitambulisha mwishoni mwa mwaka jana Steven Kanumba 'kanumba' kwa kusema hapo mwanzo kuwa yeye si mwingi wa manene bali ni kazi tu kazi tu,ndio hivyo amenza kushoot movie yake mpya mara baada ya kumaliza ziara yake HOLLYWOOD(USA),Jina la movie ni ''THE SHOCK'' Katika movie hii aeendeleza na utaratibu wake wa kutambulisha na kuibua vipaji vipya kabisa ambavyo havijawai kuonekana katika movie yoyote kama ilivyokuwa mwaka jana alipomtambulisha JENIFER,PATRICK NA PATCHO sasa katika ''THE SHOCK''..anawaleta kwenu SHAZ SADRY kwa mwaka huu ambaye ndiye mhusika mkuu katika movie hii na kwa mwaka huu mtamuona sana katika movie zangu kama msanii mpya na mwenye viwango vyote vya uigizaji bora katika filamu. alisema kanumba apapo filamu hiyo imepewa baraka zote na Kampuni ya kusambaza ya Steps Entetainment ya jijini Dar es Salaam


Waziri Mkuu wa Misri amejiuzulu

Waziri Mkuu wa Misri Ahmed Shafiq amejiuzulu
Ahmed Shafiq
Ahmed Shafiq
Baraza la jeshi lilitoa taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyekuwa waziri wa usafiri, Essasm Sharaf, amependekezwa kuunda serikali mpya.
Bw Shafiq aliteuliwa kuwa waziri mkuu siku chache tu kabla ya Rais Hosni Mubarak kujiuzulu tarehe 11 Februari baada ya siku kadhaa za maandamano
Waandamanaji walisema kuwa Bw Shafiq alikuwa mshirika wa karibu sana wa Bw Mubarak.
Baraza kuu la jeshi lilikubali uamuzi wa Bw Shafiq na kumteua Essam Sharaf kuunda serikali mpya lilisema jeshi hilo kupitia ukurasa wao wa face book.
Jumatatu, Misri ilimwekea vikwazo ya kutosafiri Hosni mubarak na familia yake.




Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini husan katika Jiji la Dar es Salaam. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 10 Machi, 2011.

Katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka wa fedha wa 2009/2010, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara wakiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA) wakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao. Maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa kati ya 172% na 200% ya viwango vya sasa.

Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.


Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA imeamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 17.9% ambapo kiwango cha nauli kwa abiria kwa kila kilomita kimepanda kutoka Sh 22.9 hadi Sh 27.

Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:

Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 150/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 300/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam .

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:

(i) Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria

(ii) Kuandika katika mlango wa kuingia abiria viwango vya nauli inavyotoza katika njia anayotoa huduma ya usafiri

(iii) Kutoa tiketi kwa kila abiria ikionyesha jina la mmiliki, namba ya usajili wa basi, kituo cha mwanzo na mwisho wa safari, nauli na tarehe ya safari

(iv) Kuzingatia usafi wa mabasi na sare za wafanyakazi wao, kutotumia wapiga debe, kutotumia lugha chafu, kutokatisha njia na kutowabugudhi wanafunzi

(v) Kubeba idadi ya abiria kulingana na uwezo wa basi na kuwepo na nafasi ya kutosha na sehemu ya kushika kwa abiria wanaosimama ndani ya mabasi makubwa

(vi) Kuhakiksha basi linabeba idadi ya abiria ambao wanapaswa kubebwa kwa mujibu wa idadi iliyoidhinishwa na mtengenezaji wa basi

(vii) Kuwepo na Bima inayowalinda abiria wote wa basi husika

(viii) Abiria wanawajibika kurejesha utamaduni wa kupanga mabasi kwa mstari na mabasi nayo yanapaswa kupakia abiria kwa mstari.

Ni vyema ikumbukwe kuwa SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji. Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.

Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine kama Ofisi ya Mkuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Manispaa, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.

Imetolewa na:

David Mziray

Meneja Mawasiliano kwa Umma

3 Machi, 2011
 

Bomu lajeruhi watu 10 Rwanda

Kagame
Rais Kagame wa Rwanda
Watu 10 wanejeruhiwa nchini Rwanda baada ya bomu kulipuka katika kituo cha basi mjini Kigali. Polisi wamesema hawajakamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hilo.
Mlipuko huo umetokea katika kituo cha basi kilichopo kwenye makutano ya barabara za Kimisagara na Nyakabanda.
Mlipuko huo ulilenga abiria waliokuwa wakiingia ndani ya basi la abiria.
Upelelezi bado unaendelea, wamesema polisi.
Mwandishi wa BBC mjini KIgali, Yves Bucyana anasema hata hivyo polisi wamekamata watu watano kuhusiana na matukio mengine ya milipuko ya mabomu nchini humo.
Polisi walisema mshukiwa mmoja alikamatwa akiwa na mabomu mawili, kati ya 15 anayodai alipewa nchini Burundi, katika mtandao wa walipuaji mabomu mjini Kigali.
Watuhumiwa hao sasa wanaongeza idadi ya watuhumiwa wa walipuaji mabomu. Tayari watu 29 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Wengi wamekiri kuhusika na vitendo hivyo wakidai kuwa waliatumwa na kundi la FDLR.
 

No comments:

Post a Comment