Pages

Pages

Monday, March 28, 2011

LINAH AJIBU HOJA ZA HADIJA KOPA

   linah akipagawisha mashabiki wa bongo flava
Msanii chipukizi wa kizazi kipya linah amejibu hoja za hadija kopa mwanamuziki mkongwe katika gemu la muziki nchini Tanzani ni baada ya kutoridhioshwa na matokeo ya tuzo ya msanii bora wa kike 2010.
   Akitujuza kwa njia ya simu mchana huu linah amesema mtu yoyote asiyekubaliana na matokeo hayo hana nia njema na kipaji chake kwani kura hakujipigia bali mashabiki ndio waliotuma sms za kuchagua linah awe mshindi wa Tuzo hiyo.
    "msanii mkubwa kama hadija kopa anatakiwa kunisaidia kwa kunishauri na sio kukosoa kwanini kakosa kupewa tuzo hiyo" alilalama linah.hata hivyo wasanii kadhaa akiwemo Lady jay dee,shaa na mwasiti wameshow love dhi ya linah kwa kumtwangia simu na kumpongeza kuchukua tuzo hiyo ambayo ilitizamwa kwa macho sabini na wasanii wa kike.
   Wadodosaji wa mambo ya huzunu na furaha wanasema kuwa Mwasiti alitoa chozi baada ya kutangazwa linah ndiye mshindi, kitu kilichowafanyawatu wengi kujiuliza je chozi lile liulikuwa ni la furaha kuskiana linah mwana  THT mwenzaqke kuchukua tuzo hiyo ama ilikuwa ni uchungu wa kukosa Tuzo hiyo.
   "Huu ni muda wa vipaji na muda wa wasanii wa kale unakaribia kuisha,huu ni muda wangu ndiyo maana watu wamenikubali zaidi yao,najua vijana wengi wananikubali sana hasa mavyuoni na mashuleni ndiko kura zangu nyingi najua zimetokea huko" alijigamba linah.
   Licha linah kutamba na nyimbo kibao amekili kutungiwa nyimbo nyingi na boyfriend wake Amini na zingine huwa anatungiwa na bosi wa Luge mutahaba,barnaba na dogo dito,hivi karibuni anatarajia kuachia ngoma kali ambayo anasema itakuwa moto wa kuotea mbali.


KIGOMA HAINA STENDI YA MABASI
   Habari za kichokonozi zinaskuwa mji wa kigoma hauna stendi maalum kwa wasafiri japokuwa wilaya zake zina stendi ambazo ni bora kuliko ya mjini humo ambo wasafiri hupata taabu kuulizia wapi basi fulani linakopaki ambapo kwa kwaida mabasi hayo hupaki mitaa tofautitofauti kutokana tajiri wa gari atakapoamua magar yake yalazwe wapi ndiko abiria huhukohuko.


     NYIMBO ZA 20% ZAONGOZA KUPIGWA KATIkA VITUO VYA REDIO NA TV
Toka 20% Apate tuzo 5 vituo vya redio na tv vimeongoza kucheza nyimbo za msanii huyo aliyevunja record ya kili music awards kwa kuondoka na tuzo 5,haijapata kutokea kila mitaa sasa ...chunga tamaa mbaya...tunarudishana nyuma kwa mambo ya kuibiana ..oooh!

No comments:

Post a Comment