Pages

Pages

Monday, March 28, 2011

TUZO ZA KILI ZIMECHAKACHULIWA-HADIJA KOPA

    Hadija kopa muimbaji wa taarabu(TOT)
  Mwimbaji wa taarabu wa siku nyingi mama yetu hadija kopa ameibuka na kudai kuwa tuzo za kili 2011 hasa katika kategori ya msanii bora wa kike mambo hayakwenda kwa kufuata haki na umuhimu wa tuzo hiyo kutokana na kiwango cha msanii aliechukua tuzo hiyo kuwa ni wazi hakustaili.
  Hayo yamesemwa leo na msanii huyo mwenye vijembe vya misemo ya pwani  katika kipindi cha "yaliomo yamo"  cha redio one,"tunataka tuone jinsi kura zinavyopigwa na wapenzi wetu kwenye hizo komputa sio kuja na vikaratasi tu na kutaja majina wayajuayo" alilalama hadija.
  Hii inatokana na kutoridhika na matokeo kwani kazi ya hadija kwa mwaka jana haifanani na uwezo wa msanii chipuzi Linna ukweli kamuacha kwa kila namna lakini mwamuzi ni kura zilizopigwa na mashabiki ambapo   Bi.Hadija anadai kuwa baadhi ya wasanii walijua siku moja kabla kuwa tayari washashinda tuzo hizo.
  Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi Bi hadija kopa hajawahi kuchukua tuzo hata moja licha yakutoa mchango mkumbwa kastika gemu la Muziki wa tanzani.
  Wachambuzi wa mambo ya sanaa nchini Tanzania wanadai kuwa lina alistaili kupata tuzo ya msanii chipukizi pekee kwani ndiko anakostaili lakini huwezi kuidondosha kipua-pua miamba kama lady jay dee,shaa,hadija kopa na mwasiti ... ...Tutamtafuta Linna atujuze kama kitoto hiki kilibebwa ama kilijitaidi kwa nguvu ya kura.Am out

Waasi wateka miji zaidi Libya

Waasi wa Libya wamechukua udhibiti wa miji mingine minne na wanasogea haraka kuelekea katika ngome ya Muammar Gaddafi katika mji wa Sirte.
Waasi
Waasi wakiwa Ras Lanuf
Waasi hao wamechukua miji ya mashariki ya Ras Lanuf, Brega, Uqalya na Bin Jawad, baada ya majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi kuodoka kufuatia shinikizo la mashambulizi ya anga kutoka kwa majeshi ya ushirika.
Waasi hao pia walidhibiti bandari ya Ajabya siku ya Jumamosi.
Ndege za Marekani, Ufaransa, Uingereza na mataisfa mengine washirika, walianza kushambulia majeshi ya serikali ya Libya siku nane zilizopita.
Nguvu za kijeshi zilifikiwa baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha hatua za kulinda raia.
Wajumbe wa Nati wanakutana mjini Brussels siku ya Jumapili, huku wakitarajiwa kujadili jinsi ya kupambana nchini LIbya na pia kuongeza shughuli zake za kijeshi.



HUDUMA YA TIBA LOLIONDO KUSITISHWA KWA MUDA

HUDUMA za uponyaji wa magonjwa sugu, zinazotolewa na Mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwaisapile, zimesitishwa kwa wiki moja,kufuatia matukio ya idadi kubwa ya watu wanaofuata tiba kufariki dunia kabla ya kupata huduma.
Mchungaji Mwaisapile maarufu Babu, aliwaambia waandishi wa habari jana hali katika Kijiji cha Samunge, sasa ni mbaya, yakiwa ni matokeo ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaofuata tiba.
Alisema hata hivyo, ongezeko la watu katika kijiji hicho limesababisha madhara makubwa ya kiafya kwa maelfu ya watu."Tumeelemewa na idadi ubwa ya watu, naomba halmashauri ya wilaya itusaidie ili tuweze kuwahudumia hawa watu ambao sasa wanakufa hata kabla ya kupata dawa," alisema.
Alisema yeye binafsi, bado ana nguvu, nia na uwezo wa kuendelea kutoa tiba kwa kadri mwenyezi Mungu alivyomjalia na kumwelekeza na kwamba anachohitaji ni ushirikiano katika kuboresha taratibu ili tiba ipatikane bila usumbufu na adha kwa wananchi.

Akisoma tamko la Mchungaji Mwaisapile, Ofisa Makazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Frederick Mwisagile, alisema linakuja baada ya kupewa taarifa kuhusu msururu wa magari uliokwama kilometa 55 kutoka nyumbani kwake.Habari zilisema msururu unakakadiriwa kuwa na zaidi ya magari 4,000 na mengine zaidi ya 100 yamekwama.

Mchungaji huyo aliiomba serikali isaidie kupunguza msongamano wa watu na magari yanaoendelea kwenda katika kijiji hicho yakitokea ndanni na nje ya nchi."Nimeambiwa watu wasiopungua 24,000 wapo ndani ya magari kwenye foleni. Najua itawachukua kati ya siku tatu hadi saba kufika kwangu, kwa kweli hali hii si nzuri na inahitaji hatua zichukuliwe haraka,"alisema.

Kwa mujibu wa mchungaji, njia ya kukabiliana na msongamano huo, ni kuhakikisha watu walioko kwenye msururu wanaisha kwanza."Naomba kuanzia leo tarehe 26 hadi Aprili mosi nishughulike na hawa waliopo kwenye foleni ili waishe kwanza,"alisitiza Mchungaji Mwaisapile.

No comments:

Post a Comment