Pages

Pages

Thursday, March 31, 2011

MTOTO WA LOWASA MBARONI KWA KUMGONGA TRAFIKI


   Edward Lowassa
liyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Bw. Bernard Lowassa (30), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma zakumgonga kwa makusudi askari wa Kikosi cha Usalama barabarani E 9320 Koplo Cyprian akiwa katika kutekeleza majukumu ya kazi.
Watu walioshuhudua tukio hilo waliaalaani na kuhoji sababu za mtoto huyo kufanya hivyo, wengine wakienda mbali zaidi wakidai pengine alifanya hivyo kwa kujiona hawezi kubanwa na sheria kwa kuwa ni mtoto
wa kigogo.
Tuko hilo lilitokea juzi saa 1 jioni eneo la Namanga, Oysterbay  katika eneo la taa za kuongoza magari.
Akiendesha gari lenye namba za usajili T 573 BQV, Corona Primio, kutoka Msasani kwenda Morocco, alikaidi utaratibu wa trafiki huyo wa kuruhusu magari kupita kwa awamu kwa kulazimisha kupita kabla hajaruhusiwa.
Koplo Cyprian pengine kwa lengo la kuepusha magari kugongana na kutaka kuchukua hatua ukaidi wa Bernard, alilazimika kumzuia asipite lakini, bila kujali wala woga, aliendesha gari lake na kumgonga katika mguu na kumsukuma.
Mshuhuda walioshuhudia tukio hilo walisema askari huyo aling'ang'ania gari hilo hadi madereva wengine walipomuokoa kwa kulizuia gari la kijana huyo baada ya kusimama mbele ya gari lake.
Baada ya madereva wengine ambao nao walikuwa wakisubiri kuruhusiwa kupita katika taa hizo kukerwa na kitendo alichokifanya Bernard kumugonga kwa makusudi.
Watu wakiwa na hasira nusura wamshushie kipigo mtoto huyo lakini, askari huyo liwasihi wasifanye hivyo bali waiache sheria ichukue mkondo wake.



 WAPIGANAJI WA I VORY COAST  WAELEKEA MJI MKUU

 

Majeshi yanayomtii Bw Ouattara
Majeshi yanayomtii Rais anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa Alassane Ouattara yanaelekea kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Yamoussoukro.
Majeshi yake hivi karibuni yameteka miji kadhaa na kiongozi aliye madarakani Laurent Gbagbo ametaka mapigano yasitishwe.
Bw Gbagbo amekataa kuachia madaraka licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa Novemba.
Mwandishi wa BBC alisema Yamoussoukro ni mji mkuu tu kwa jina, lakini kutekwa kwake kutakuwa ni ushindi wenye umuhimu mkubwa kwa majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara.
Takriban watu 1,000,000 wamekimbia mapigano- hasa katika mji mkuu Abidjan- na karibu 462 wameuawa tangu Desemba, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Katika mji wa magharibi wa Duekoue, maelfu ya watu wamejihifadhi kwenye kanisa baada ya kukimbia mapigano wiki hii.



JUHUDI ZA MENGI ZA GONGA MWAMBA MAHAKAMANI
mengi
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imerejesha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jalada la kesi ya madai ya fidia ya Sh1, inayomkabili Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi na kuagiza kesi hiyo iendelee kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana.
Jalada hilo lilitishwa katika mahakama kuu na Jaji Mfawidhi, Semistocles Kaijage,  kufuatia ombi la Mengi kupitia kwa wakili wake, Michael Ngalo.
Katika ombi hilo, Mengi alilalamikia kile alichodai kuwa ni kutokuridhishwa na namna hakimu Aloyce Katemana, anavyondesha kesi hiyo.Malalamiko hayo yalikufuatia tukio la   Februari 11 mwaka huu, wakati haki huyo, alipozikataa nyaraka 14 zilizowasilisha  na Mengi ili ziwe sehemu ya vielelezo vya ushahidi katika utetezi wake.
Februari 23 mwaka huu, wakili wa Mengi, Ngalo alindika barua kwenda  Mahakama Kuu ya Tanzania, akilalamikia jinsi hakimu Katemana anavyoiendesha kesi hiyo.Alidai kuwa hakimu huyo alikuwa analia upande mmoja na kwamba hata uamuzi wake ulikuwa wa mashaka.
Wakili huyo alimuomba Jaji  Kaijage, alipitie jalada la kesi hiyo.Hata hivyo habari zilizopatikana jana zilisema baada ya kupitia jalada hilo, Jaji Kaijage, aliridhika kuwa hakuna ukiukwaji wa sheria wala taratibu katika uendeshaji wa kesi hiyo na hivyo kuagiza jalada lirejeshwe katika Mahakama ya Kisutu, ili kesi iendelee kusikilizwa mbele ya hakimu Katemana.
Pamoja na kurejesha jalada hilo, jaji Kaijage pia alimtaka wakili Ngalo kama atakuwa ,  awasilishe ombi   katika Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu, ombi la kutaka hakimu huyo ajitoe kusikiliza kesi hiyo



Waziri wa mambo ya nje wa Libya aasi na kukimbilia Uingereza


 KATUNI YA GASSAFI

Waziri wa mambo ya Nje wa Libya , Moussa Koussa ameasi na kukimbilia Uingereza kutafuta hifadhi.Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, mwanadiplomasia huyo pia amejiuzulu. Kwa upande mwengine ; huko Libya kwenyewe, vikosi vinavyomtii Kanali Muammar Gaddafi vinaripotiwa kuwashambulia waasi na kuwalazimisha kuikimbia miji kadhaa waliokuwa wakiidhibiti katika kipindi cha siku mbili zilizopita.
 Waasi hao wameshindwa nguvu hata baada ya wanajeshi wa kigeni wanaoongozwa na NATO kuendelea na operesheni ya Odyssey New Dawn inayoingia siku yake ya 10.Hata hivyo,Waziri Mkuu wa Uingereza aliashiria hapo jana Jumatano kuwa uwezekano wa kuwapa silaha waasi hao upo.
Duru zinaeleza kuwa vikosi vinavyomtii Kanali Muammar Gaddafi vinawashinda nguvu waasi hao.

No comments:

Post a Comment