Pages

Pages

Saturday, April 16, 2011

DR SLAA KUTAJA ORODHA NYINGINE YA MAFISADI TABORA

 Dr Willibrod Slaa

  Duru za siasa nchini Tanzania zinasema baada ya Chama cha Mapinduzi kuwataka wanaojijua mafisadi ndani ya chama hicho kujiondoa na kujivua gamba ndani ya siku 90, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo ataweka hadharani orodha ya pili ya majina ya watuhumiwa mafisadi baada ya ile ya awali aliyoitoa mwaka 2007, Mwembeyanga.
        Septemba 15, 2007, Dk. Slaa akiwa wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mwembeyanga aliwataja vigogo 11 wanaodaiwa kuwa ni mafisadi akiwemo aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Nchini (BOT) ambaye sasa ni marehemu Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge, na Basil Mramba aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Rombo.
       Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina; Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Patrick Rutabanzibwa; Kada wa  Nazir Karamagi; mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono ; mbunge wa Igunga Rostam Aziz ; mbunge wa Monduli Edward Lowassa ; Rais mstaafu wa Awamu ya ....,na....
        Dk. Slaa ambaye yupo mkoani Tabora akiongozana na viongozi wengine katika ziara ya kukijenga chama mkoani humo atafanya mkutano wa hadhara na kutaja orodha hiyo mpya baada ya CCM kushindwa kutaja majina ya mafisadi hao.


MBWANA SAMATTA KUUZWA KWA MILIONI 150 TP MAZEMBE
 Msukuma kabumbu wa timu ya simba Mbwana Samatta amenunuliwa na timu ya DRC ya Tp mazembe kwa dola kimarekani zenye thamani na milioni 150 za kibongo na tajiri wa timu hiyo ambaye ni Gavana wa jimbo la katanga na mmliki wa migodi ya dhabu nchini DRC.

William Ruto afutiwa mashitaka ya ufisadi

 

Mahakama Kuu nchini Kenya imefuta mashtaka ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili waziri wa zamani wa elimu ya juu, William Ruto, baada ya kukosekana kwa ushahidi. Ruto ni miongoni mwa wanasiasa wanaoshitakiwa pia na ICC.


            Ruto na watu wengine wawili walikuwa wakituhumiwa kuliibia  Shirika la Usafishaji Mafuta la Kenya zaidi ya dola milioni 1 kwa kuliuzia ardhi ya eneo la hifadhi ya misitu.
Uamuzi wa kumvua Ruto kwenye mashitaka hayo, unakuja siku moja tu baada ya mwanasiasa huyo kurejea nyumbani kutoka  kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu, kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi hapo mwaka 2007.
          Swala kubwa ambalo hivi sasa watu wengi nchini Kenya wanajiuliza, ni iwapo Ruto atarejeshwa katika nafasi yake ya uwaziri. Aboubakar Lyongo amezungumza na mwanasheria wa kujitegema, Harun Ndubi, kutaka ufafanuzi zaidi wa kisheria katika suala hilo.
      

No comments:

Post a Comment