Pages

Pages

Monday, April 18, 2011

DR.SLAA AWALIZA WATU BAADA YA KUMUWEKA DR.MAGUFULI MSALABANI

            
              Chambuzi za mambo za siasa nchini Tanzania zinasema kuwa Dr.slaa ameumiza sana mioyo ya watu baada ya kumtaja kipenzi cha watu Dr.John Magufuli kama moja wa watuhumiwa wa ufisadi katika serikali ya mpendwa wetu JK.
             Wachunguzi wa mambo ya isiasa wanasema kuwa kauli hiyo iliwaumiza watanzania wengi kutokana watu wanavyomkubali sana kiongozi huyo kwa utendaji wake wa umakini na mtu asiyeyumbishwa na mambo ya tamaa ya uongozi,hii imewaumiza pia wapiga kura wa jimbo la chato anakotoka Mh.Magufuli.
               Hii ilikuwa siku ya jumamosi ambapo Dr slaa akiwa Tabora aliwataja waheshiwa wengine kama Mangula.Malicela,sumaye n.k ambao wamo katika orodha hiyo mpya.




 SHAKIRA AIBIWA PETE JUKWAANI                               Shakira akitoa shoo ya nguvu kwa mashabiki
         Mwanamuziki maarufu duniani,Shakira ameibiwa pete yake ya thamani wakati alipokuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake waliohudhuria shoo yake nchini Mexico
         Shakira alikuwa akipiga shoo katika chuo kikuu cha University of Monterrey kilichoko kwenye mji wa Monterrey-Mexico wakati kibaka mmoja alipofanikiwa kuivua pete ya nyota huyo wa muziki wa Pop Shakira ambaye alikuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake,aligundua muda mfupi baadae kuwa pete yake ameishavuliwa,lakini Shakira hakukatisha shoo yake na wala hakumkamata mwizi wake na mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa kutokana na tukio hilo.



 
Arsenal sare 1-1 na Liverpool

Wachezaji wakisikitika baada ya matokeo
             Matumaini ya Arsenal ya kutwaa ubingwa msimu huu, yamevurugika kwa mara nyingine baada ya kufungwa bao la mkwaju wa penalti la kusawazisha dakika ya mwisho ya mchezo, walipokumbana na Liverpool katika uwanja wa Emirates
             The Gunners walikuwa wamekwishafikiria wamevuna pointi tatu muhimu kutokana na mkwaju wa penalti aliofunga Robin van Persie dakika ya 96 baada ya Jay Spearing kumuangusha chini Cesc Fabregas ndani ya sanduku la hatari.
             Lakini ikiwa imesalia dakika moja mpira haujamalizika, Emmanuel Eboue alimchezea rafu Lucas Leiva kwa kumsukuma na Dirk Kuyt akafunga kwa mkwaju mkali wa penalti na kuisawazishia Liverpool.
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal iwe nyuma ya Manchester United kwa pointi sita, huku ikiwa imesalia michezo sita kabla ligi haijamalizika kwa msimu huu.



VIDEO YA STL HABA HABA NCHINI NNORWAY

    Kwa sasa STL anajiandaa kwa ajili ya nusu fainali ya The Eurovision music contest itakayofanyika May mjini Dusseldorf,Ujerumani huku akiwa na mwalimu wake wa anayehakikisha kuwa anakua fiti kwenye shindano hilo.



JAPHET KASEBA ADUDWA NA KUJIUZULU NDONDI

  Bondia alieibukia toka kwenye kick boxing Kasebaseba,uzi usiku wa kuamkia jana alidundwa na Maugo kwa TKO,kipigo hiko kilimpelekea kujiuzulu ndondi na kurudi kwenye fani yake ya kick boxing.



GAMBA JIPYA...SUMU ILEILE!!

NI mwendo wa kujivua gamba kwa staili hii...

No comments:

Post a Comment