Pages

Pages

Saturday, April 2, 2011


MAGUFULI USO KWA USO MCHUNGAJI WA LOLONDO NA KUMIMINA BILLIONI 1

Waziri wa ujenzi John Magufuli akinywa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Masapila katika kijiji cha Samunge, Loliondo mkoani Arusha

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana aliingia katika Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila na kupata kikombe cha dawa, kisha kutangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.
Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali itatumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.
Barabara inayoingia katika kijiji hicho ambacho kimeshuhudia maelfu ya magari yakiingia kila siku tofauti na ilivyokuwa awali, ipo katika hali mbaya kiasi cha baadhi ya maneo kutoruhusu magari kupishana.
Kwa mujibu wa Magufuli, Serikali ilikwishatoa Sh500/-milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu eneo la Kigongoni, Ngaresero, Samunge hadi kuungana na barabara ya kutoka mkoani Mara.
Dk Magufuli alisema jana ndio aliuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Makao Makuu kutuma Sh500 milioni ili kuharakisha ujenzi huo.
"Tayari fedha hizo zimeshatumwa Tanroads mkoani Arusha na Meneja wa Mkoa, Kakoko (Deodatus), niko naye hapa hivyo kazi itakwenda haraka ili watu wanaokuja kwa mchungaji kunywa dawa wasiendelee kuteseka," alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwa wakimsikiliza.
Waziri pia huyo alisema kwa mamlaka aliyonayo, atawasiliana na uongozi wa Mfuko wa Barabara ili utume fedha za dharura kiasi cha Sh50 milioni kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorogoro kwa ajili ya kufanya matenegenezo mengine ya barabara, wilayani humo.
Alisema fedha zilizotengwa kwa ajilii ya barabara za nchi nzima kupitia mfuko huo zinafikia Sh286 bilioni katika bajeti ya mwaka 2010/11, na kwamba upo uwezekano mkubwa wa fedha za dharura kupatikana kwa ajili ya matenegenezo ya barabara ya Samunge.
 
 
 SHAKIRA ATUPIWA MBICHI NA G.PQUE
 c    Shakira na Pique kama wanavyoonekana  wana uhusiano wa kimapenzi ambao sasa umewekwa wazi kwa kutolewa picha za wawili hao katika vyombo vya habari na ikichukuliwa kuwa Barcelona na Real Madrid ni watani wa jadi ,inaelezwa kuwa klabu hiyo ya Blancos  imeamua kutotoa nafasi ya nyimbo za nyota huyo  mwenye umri wa miaka 34 kupigwa kwenye uwanja wake,taarifa kutoka katika vyombo vya habari  zinadai kuwa hakuna wimbo wowote wa mwanamuziki huyo utapigwa
 

MREMBO JULIETH AKABIDHI FEDHA KWA WANAFUNZI WALEMAVU WA NGOZI


MISS Progress Internatinal Julieth Wiliam Lugembe ambaye ni mkurugenzi wa Progressive Foundation, ametoa shilingi milioni 1.4 kwa walemavu wa ngozi wa Wilaya wa Ilala.

Julieth alikabidhi fedha hizo kwa mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi mbele ya mwakilishi wa afisa wa ustawi wa jamii manispaa ya Ilala Rachel Katemi.

Fedha hizo alizitoa kwa ajili ya kununua sare za shule za watoto hao wa shule za msingi wapatao 30.
Mrembo huyo ambaye ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Progress Foundation amejitolea fedha hizo kutoka mfukoni mwake ili kusaidia watoto hao.
Julieth alisema kuwa ameamua kuwasaidia watoto ili wapoate elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine wasio na ulemavu.
“Lengo langu ni kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili waweze kufikia malengo yao ya kielimu kama wototo wengine ambao hawana ulemavu wowote,” alisema Julieth.
Mlimbwende huyo alitwaa taji hilo la Miss Progress Internatinal katika shindano lililofanyika nchini Italia baada ya kuwashinda warembo wengine kutoka nchi zipatazo 60. 
 
 
PALIPO NA MIZIGO HAPAKOSI USAFIRI
Mikakati yakutimiza malengo ya milenia 2025 
 

Mji mkuu wa Ivory Coast wazingirwa

Majeshi yanayomtii Rais wa Ivory Coast anayetambuliwa na jumuiya za kimataifa , Alassane Ouattara, yamezingira mji mkuu wa Abidjan kutoka maeneo mbalimbali
Hatua hiyo inatishia kusababisha mapambano kwenye mji huo, ngome ya mwisho ya Rais mpinzani Laurent Gbagbo.

Majeshi yanayomtii Ouattara
Awali mkuu wa majeshi wa Bw Gbagbo aliomba hifadhi kwa balozi wa Afrika Kusini.
Umoja wa Mataifa umesema Bw Gbagbo alishindwa kwenye uchaguzi mwaka jana, lakini amekataa kukabidhi madaraka kwa Bw Ouattara.
Majeshi yanayomwuunga mkono Bw Gbagbo yamekuwa yakishika doria kwenye wilaya za mji huo, na kuweka vizuizi vya barabarani.
Mwandishi wa BBC Valerie Bony mjini Abidjan alisema kumekuwa na mapigano makali kwenye kituo cha televisheni cha taifa liliopo eneo wanalokaa wakazi, na milipuko kwenye vitongoji kaskazini mwa nchi hiyo.

Lindsay Lohan -- I Wasn't Drunk When I Got Tipsy!

 Lindsay Lohan says she was NOT loaded on grandpa's cough medicine -- aka booze, hooch, or liquor -- when she busted her butt in NYC ... telling TMZ flat-out, "I was NOT drinking, nor do I drink!"

0331_lindsay_excl
LiLo is on the defensive after being photographed going down hard outside the Motor City Bar on Wednesday -- because some people had the audacity to think Lindsay Lohan falling down outside a bar may mean she fell off the wagon.
But that's not the case ... because Lohan tells TMZ, "I was with my brother, sister and friends. I was making a joke. They're trying to make something out of nothing."
Lindsay adds, "Just because I'm out doesn't mean I'm drinking."

No comments:

Post a Comment