Pages

Pages

Tuesday, April 5, 2011

SUMAYE ACHARUKA ASEMA SIASA SI DOLA

WAKATI CCM ikitaka dola ikidhibiti Chadema, Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu, Fredrick Sumaye, amekitaka chama hicho tawala kukabiliana na hoja za Chadema kisiasa badala ya kuiachia Serikali ipambane nao.

Juzi CCM kilisema nyendo za Chadema zina agenda ya siri ya kuking’oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha katiba hivyo kiliitaka Serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.

“CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria… Wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi. “Wanachochea wananchi wakisema, ‘peoples’  na hujibu ‘power’! (nguvu ya umma), Je mpo tayari kufanya kama Tunisia, Misri? (ambako serikali zilipinduliwa kwa nguvu ya umma)”  alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika juzi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili bila kujua kwamba CCM wangekuwa wanazungumzia suala hilo, Sumaye alisema CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za Chadema na si kuiachia Serikali ipambane nao.

Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si serikali, hivyo CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Chadema kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.Sumaye alisema si ishara nzuri kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaendelea kukishtaki kwa wananchi kuwa kimeshindwa kufanya kazi.

Sumaye ambaye Mwananchi Jumapili ilimtafuta kusikia maoni yake kuhusu mfululizo wa mikutano ya Chadema na mustakabali wa CCM, alisema chama hicho tawala kinapaswa kujibu hoja zote za Chadema kisiasa na kama hakina majibu kiiombe Serikali majibu hayo na iyatoe kwa wananchi.



VIKOSI VYA BAGBO VYAPIGWA MABOMU
vikosi vinavyomuunga mkono Bw Ouattara
Vikosi vinavyomuunga mkono Ouattarra vimeimarisha mashambulizi dhidi ya Gbagbo
Ndege za kijeshi za Ufaransa na za Umoja wa mataifa zimeshambulia kambi za kijeshi zinazotumiwa na Laurent Gbagbo mjini Abidjan.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Hamadoun Touré amesema ndege hizo zimelenga kuharibu makombora yanayotumiwa na jeshi la Gbagbo dhidi ya raia na vikosi vya umoja wa mataifa.
Mkaazi mmoja mjini Abidjan aliyeshuhudia harakati hizo za wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa amesema nyumba yake ilitikiswa na mabomu hayo.
"Nilikuwa nyumbani mwangu, kisha nikasikia helicopter ya kijeshi ikipaa chini sana, ilinibidi nitoke nje kutizama ndipo nikaona ilikuwa ya jeshi la ufaransa. Kisha baada ya muda wa saa moja hivi nikasikia mrindimo wa mabomu na nyumba ikawa inatikisika."
Mkaazi huyo amesema kambi ya kijeshi ya Aqedo ilikuwa inashambuliwa. Na ameelezewa na wenzake kutoka sehemu zingine mjini Abidjan kuwa wao pia wamesikia sauti za milipuko kwenye kambi za kijeshi.
Kwa upande wake waziri wa mashauri ya kigeni katika serikali ya Laurent Gbagbo, Alcide Djedje ameiambia BBC kuwa wanajeshi wa umoja wa mataifa na wale wa ufaransa wanashambulia raia.
Madai hayo yamekanushwa na Umoja wa Mataifa.
Navyo vikosi vinavyomuunga mkono Alassane Ouattarra vimeongeza juhudi zao za kudhibiti mji wa Abidjan.
Waziri mkuu Guillaume Soro amesema sasa wapo kwenye mkondo wa mwisho na katika siku chache tuu watadhibiti utawala wa Ivory coast.
"Tumefurahishwa na harakati za wanajeshi wetu. Mpango ulikuwa kuuzingira mji wa Abidjan na wamefaulu vizuri sana." amesema Waziri Mkuu Soro.
Wakaazi wengi mjini Abidjan wamelazimika kujifungia nyumbani na hawana vyakula, maji na huduma ya umeme.

JENNIFER LOPEZ TWEETS PICS FROM HER 'I'M INTO YOU' VIDEO SHOOT

Jennifer Lopez is currentlylbum drops on May 3.

  SANAMU YA MUSEVEN WAMUWEKA KATIKA UTATA GRACE NAKIMERA

Grace Nakimera toka Uganda huenda akajikuta yuko kwenye matatizo na maafisa wa Ikulu ya Uganda kutokana na wimbo wake mpya uitwao Bagalaki featuring Aziz Azion

Tatizo linaanzia pale Grace Nakimera alipotumia taswira za Presidaa Museveni na Kiiza Besigye wakicheza kwenye video yake na kusemekana kuwa maafisa ya Ikulu hawajafurahishwa na kitendo hicho cha kutumia sura ya Prezidaa kama katuni na ni kama wamemkejeli!...kwenye video hiyo kuna mtu amevaa kama Museveni na anacheza karibu na Basigye na kwa sasa maafisa wa ikulu ya Uganda wanangoja maelezo toka kwa Grace Nakimera

Rooney akabiliwa na adhabu kwa kutukana

Wayne Rooney anakabiliwa na adhabu ya kukosa mechi mbili, kutokana na kosa la kutumia lugha chafu wakti Manchester United ilipokutana na West Ham.
Rooney
Wayne Rooney akitukana mbele ya kamera
Mshambuliaji huyo wa United alitukana mbele ya kamera iliyokuwa ikirusha picha za moja kwa moja, baada ya kupachika bao la tatu kwenye uwanja wa Upton Park.
Mashambuliaji huyo pia wa England ana mpaka Jumanne jioni kukata rufaa dhidi ya shitaka hilo la chama cha soka cha England.
Iwapo atakiri kosa hilo, atapatiwa adhabu hiyo ya kutocheza mechi mbili, lakini iwapo atakana mashitaka hayo, shauri lake litasikilizwa siku ya Jumatano.
Adhabu ya kukosa mechi moja itamkosesha kucheza dhidi ya Fulham siku ya Jumamosi, huku akipatiwa adhabu ya mechi mbili, atakosa mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City, kwenye uwanja wa Wembley Aprili 16.

The Game: Why Chevy Took My Corvette Away


The Game was surrounded by a bunch of BADASS cars in Hollywood yesterday ... but not one of the rides was his tricked out Corvette ... because that whip was repossessed a few days ago ...  has learned.

040411_the_game_video
Game tells  he leased the Corvette roughly three years ago ... but he was on tour when the lease expired and was unable to return it.

040411_the_game_corvette_dubs
But a few days ago, after Game returned home, repo men came to the house and took the car away. Sources connected to the situation tell us Game was home at the time and was "cooperative" during the hand-off. 

Wachina Watengeneza Ng'ombe Wanaotoa Maziwa ya Binadamu


Maziwa ya binadamu toka kwa Ng'ombe yako njiani
    
Wanasayansi wa nchini China wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa kama yale yanayotolewa na wanawake wanaonyonyesha.
Wanasayansi wa nchini China wametamba kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe 300 wanaotoa maziwa kama ya BINADAMU.

Katika ripoti ya wanasayansi hao iliyotolewa kwenye jarida la Public Library of Science One journal, wanasayansi hao walisema kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa yenye protini ya Lysozyme ambayo hupatikana kwenye maziwa ya binadamu pekee ambayo humwezesha mtoto kuweza kujilinda na maradhi mbalimbali.

Wanasayansi hao waliifanyia marekebisho embryo ya ng'ombe na kisha kuipandikiza mimba kwenye ng'ombe jike ambaye alipozaa alizaa ng'ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kama ya binadamu.

"Maziwa haya ni tofauti kabisa na maziwa ya kawaida ya ng'ombe, yana ladha tofauti na maziwa ya ng'ombe", alisema Profesa Ning Li, kiongozi wa utafiti huo katika chuo kikuu cha China Agricultural University.

"Tuna malengo ya kuuza baadhi ya tafiti za ugunduzi huu ndani ya miaka mitatu ijayo", alisema Profesa Ning Li na kuongeza " Itachukua kama miaka 10 kabla ya watu hawajaanza kununua maziwa ya binadamu madukani".

Profesa Li aliongeza kuwa maziwa hayo yatakuwa na virutubisho vingi muhimu kwa mwili wa binadamu.

Hata hivyo utafiti huo umewagawanya watu ambapo baadhi wanaupinga huku wengine wakiuunga mkono.

"Tuna wasiwasi mkubwa na utafiti huu wa kuwafanyia marekebisho ng'ombe na kuwapandikiza vinasaba vya binadamu", alisema Helen Wallace, mkurugenzi wa GeneWatch UK.

"Kuna maswali mengi kama maziwa haya yatakuwa salama kwa binadamu, inabidi yafanyiwe majaribio makubwa kama majaribio yanayofanywa kwa madawa katika kuchunguza kama yatakuwa hayana madhara kwa binadamu", aliongeza bi Helen Wallace.

Hata hivyo Profesa Keith Campbell, mtaalamu wa baiolojia katika chuo kikuu cha University of Nottingham nchini Uingereza amepingana na bi Helen na kusema kuwa kama taratibu zote za kitaaluma kuhusiana na vinasaba zitatumika maziwa hayo hayatakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.

Mwanamuziki Martelly ashinda uraisi wa Haiti

Michel Martelly
Mwanamuziki Michel Martelly ameshinda uraisi wa Haiti, akimpita kwa mbali sana mpinzani wake kwenye uchaguzi wa marudio, mke wa zamani wa rais wa nchi hiyo, Mirlande Manigat.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Baraza la Uchaguzi la Haiti yanampa Martelly karibu asilimia 68 ya kura na, hivyo, kumsafishia njia ya kungia ikulu ya taifa hilo masikini lililooko katika Bahari ya Caribbean.
Vifijo na nderemo zilisikika kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, mara tu baada ya matangazo kutolewa, huku vijana, ambao wengi wao walimuunga mkono muimbaji huyu wa muziki wa pop, wakiwasha fashifashi.
Akitumia mtandao wa Twitter, Martelly aliwashukuru wapiga kura wake akirudia ahadi yake ya kushirikiana na Wahaiti wote kuijenga nchi yao, ambayo hadi sasa haijatoka kwenye maharibiko ya tetemeko la ardhi la mwaka jana.
"Serikali nitakayoiongoza itaweka umuhimu zaidi katika muundo kuliko fedha. Tunahitaji msaada, tunahitaji mashirikiano, tunahitaji mafunzo, tunahitaji kubadilisha ufahamu wetu, maana kwa sasa tuna akili za kujiharibu wenyewe." Amesema.
Rais asiye na uzoefu wa siasa
Wafuasi wa Michel 'Sweet Micky' Martelly wakibeba bango la kiongozi huyo Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Wafuasi wa Michel 'Sweet Micky' Martelly wakibeba bango la kiongozi huyoAkijuilikana zaidi kwa jina lake la kisanii la "Sweet Micky", Martelly alitumia muda mwingi wa kampeni zake kuahidi mabadiliko kwa mfumo mzima uliopo, ambao unashutumiwa kwa ufisadi na utawala usiojali sheria. Mara nyingi alipanda jukwaani na kutumbuiza kwanza kwa nyimbo zake kabla hajahutubia.
Martelly anatambuliwa kama mwanamuziki mwenye vituko awapo jukwaani, ikiwa ni pamoja na kuvaa nywele za bandia na kuvua nguo zake. Hana uzoefu wowote wa  siasa, na hajawahi kushika nafasi yoyote serikalini.
Lakini wachambuzi wanasema kuwa, kwa Wahaiti kumchagua msanii huyu asiye na uzoefu kwenye siasa na kumuwacha Manigat, ni dalili ya kuvunjika moyo kwa wapiga kura wa nchi hiyo na wanasiasa wao.
Licha ya kuwa haya ni matokeo ya awali tu, ambayo yanaweza kupingwa kisheria, lakini tafauti kubwa ya kura kati ya Martelly na Manigat, inaondoa uwezekano wa kuwa na rais mwengine asiyekuwa mwanamuziki Martelly kwa Haiti.
Changamoto kubwa
Jengo la ikulu ya Haiti lililoharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi la 2010 Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Jengo la ikulu ya Haiti lililoharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi la 2010Sasa Martelly anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuijenga mpya nchi yake, ambayo imeharibiwa kabisa, sio tu na tetemeko la ardhi la Januari mwaka 2010, lililogharimu zaidi ya vifo 300,000, bali pia na uchumi ulioporomoka kabisa. Hadi sasa maelfu ya wahanga wa tetemeko hilo wangali wanaishi kwenye kambi za dharura.
Umoja wa Mataifa na serikali za nchi fadhili, ambazo zimemimina mabilioni ya dola kuijenga nchi hiyo, zinataka kuona uchaguzi huu unatoa serikali iliyotulia na uongozi halali wa kuchukua dhamana ya ujenzi mpya wa nchi.
Marekani yapongeza
Rais Barack Obama wa Marekani Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Rais Barack Obama wa MarekaniMarekani imewapongeza Wahaiti kwa uchaguzi huu, ambao imeuita hatua muhimu sana. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ubalozi wa Marekani nchini Haiti umesema kwamba, tafauti na chaguzi zilizopita, wa mara hii umekuwa na rekodi ndogo kabisa, ya ukiukwaji wa taratibu, na, hivyo kuwataka wale wote watakaolalamikia matokeo yake, kufanya hivyo kwa njia za kisheria na kisiasa.
Vikiwa vinachelea machafuko, vikosi vya Umoja wa Mataifa vimekuwa vikiweka doria kwenye mitaa ya mji mkuu Port-au-Prince na miji mingine muhimu ya nchi hiyo. Baadhi ya maduka bado yamefungwa kwa khofu hiyo hiyo ya machafuko. 


MARYA AMPIGA KIBUTI COLONEL MUSTAFA SABABU YA DINI

Prezenta maarufu nchini Kenya aka king of radio,Shaffie Weru inasemekana kuwa amemchumbia kwa siri,Artist toka Ogopa DeeJayz Mary Maina aka Artist Marya kwenye tukio lililofanyika mjini Mombasa


MARYA NA COLONEL MUSTAFA....ENZI HIZO
Marya alikua ni girlfriend wa Artist toka Deux Vultures,Colonel Mustafa tangu mwaka 2006 hadi uhusiano wao ulipoingia doa kutokana na pressure ya wazazi,kutokana na tofauti za kidini

MARYA AKIWA SHAFFIE 
Colonel Mustafa ni Muislam,wakati Marya ni Mkristo na kwa sasa kila mmoja ameshabadilisha kwenye Facebook accounts zao kipengele cha mahusino na vinasomeka kuwa single na Marya kufunguka zaidi kwenye Facebook kuwa amechoka kuishi kwa pressure,na ni mdogo kwa umri kuishi kwa pressure
Naye ex-boyfriend wa Marya,Colonel Mustapha ameshangaa kusikia story hizo za kuvalishana pete kwa Marya na shaffie Waweru na kuhoji kwani Shaffie ambaye ni rafiki wake wa karibu kufikia kumwita kaka ni muislam kama yeye sasa anashangaa tatizo lilikua ni dini au jingine?

Rihanna Signs To Roc Nation & Starts Rihanna Entertainment!

Rihanna has left her longtime manager, and signed with the management arm of Jay-Z's Roc Nation.

Just weeks before her highly-anticipated new album, 'Loud,' hits stores, Rihanna has announced that she will now be represented by Jay's company, alongside fellow singer Melanie Fiona, producer Mark Ronson and rapper Wale.

"[I'm] so excited to take this next step in my career," Rihanna told the Associated Press.


The move to Roc Nation is unsurprising, as Jay has served as Rihanna's mentor for the past five years, having signed her to Def Jam back in 2005, while briefly serving as the label's president.


In addition to signing with Jay's management company, the Barbados-born singer also revealed that she's started her own company, Rihanna Entertainment, to "merge all of her businesses, including music, film, fragrance, fashion and book ventures."

No comments:

Post a Comment