Pages

Pages

Monday, April 4, 2011

UN-MAUAJI YA IVORY COAST YANATISHA

Wapiganaji wa Ouattarra
Alassane Ouattarra amekanusha kuwa kundi lake linahusika na mauaji Duekoue
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea mshtuko wake kufuatia taarifa za mauaji ya mamia ya watu mjini Duekoue magahribi mwa Ivory Coast.
Ban Ki Moon amemtaka Alassane Ouattarra anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kama mshindi wa kura za Urais nchini humo, afanye uchunguzi kufuatia tetesi kuwa wafuasi wake wanahusika na mauaji hayo.
Bw Ouattarra hata hivyo amekanusha madai kuwa wapiganaji wanaomuunga mkono wanahusika na kisa hicho.
Taarifa za awali za Umoja wa Mataifa zinasema watu 330 waliuawa.
Vikosi vya kulinda usalama vya Umoja huo sasa vinawalinda maelfu ya watu waliokimbilia hifadhi katika kanisa moja mjini Abidjan baada ya mapigano kuchacha.
Wakaazi mjini humo wanasema hali imetulia kwa sasa lakini kuna amri ya kutotoka nje ambayo inatekelezwa.
Wapiganaji wanaomuunga mkono Bw Ouattarra wamefaulu kudhibiti maeneo mengi nchini humo tangu mashambulizi dhidi ya Gbagbo na wafuasi wake yaanze wiki iliopita.
Taarifa zinasema kuwa mkuu wa majeshi Philippe Mangou, ambaye alitangaza kujiunga na Bw Ouattarra wiki iliopita, ametoka kwenye ubalozi wa Afrika Kusini alipoomba hifadhi.
Jenerali Mangou sasa amekubali kurejelea majukumu yake baada ya kufanya mazungumzo na Laurent Gbagbo.
Taarifa zingine zinasema kuwa Umoja wa Mataifa unapanga kuwahamisha wafanyikazi wake 200 walioko mjini Abidjan.

AC MILAN YAIGONGA 3-0 INTER MILAN

TIMU ya AC Milan imejiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A baada ya kuwatandika Inter Milan kwa mabao 3-0 na kuongeza
pengo la pointi tano dhidi ya mahasimu wao.
Katika mechi hiyo ya juzi, mchezaji Alexandre Pato ndiye aliifungia timu yake mabao mawili huku beki, Cristian Chivu akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Mbrazil huyo mapema kipindi cha pili.
Pato alipachika bao lake dakika za kwanza za mchezo huo kabla ya kupachika la pili, muda mfupi baada ya Inter Milan kubaki na wachezaji 10 uwanjani.
Bao la tatu na la ushindi lilifungwa  na Antonio Cassano kwa mkwaju wa penalti, ikiwa imesalia dakika moja mpira umalizike.
“Tulibaki kuwa watulivu na kucheza soka,” alisema Allegri. “Hatukuwaachia Inter wapate nafasi nyingi za kufunga na kwa upande wetu pia tulipata nafasi nyingi," aliongeza mchezaji huyo.
Timu zote mbili zimebakiza mechi saba na Inter Milan, huenda ikapitwa na Napoli kama itakuwa imeshinda mechi yake ya jana dhidi ya Lazio.

 

GRACE NAKIMERA ADATISHA MIDUME DUBAI!


Msanii Grace Nakimera toka Uganda alikua na wakati mgumu alipokua Dubai hivi karibuni kwa showz kadhaa aka series of concerts.
Kuna show moja alipiga pande za Club Dhow Palace,alikutana na wanaume wenye uchu coz baada ya kuwaburudisha walimsubiri nje ya hoteli hiyo wakimtaka kimapenzi
Kilichomsaidia ni security walimsaidia kutoka nje ya hotel,ila njemba hizo bado zilitaka contact za Grace Nakimera au japo namba ya chumba alichofikia....Duh!

Lil Wayne falls in deeper tax hole

Photobucket
Platinum-selling hip-hop star Lil Wayne is in town tonight, live at the Palace. Don't be surprised if the IRS is waiting backstage to collect on a brand new $5.6 million tax bill.
The IRS filed the enormous tax lien against him Monday in Miami.
Seems Lil Wayne, real name Dwayne Carter, can't shake the tax man. In December, he paid off a $1.13 million federal tax lien, only to fall even deeper in debt this time.

 WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI AJIUZURU
Guido Westerwelle

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amejiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa chama cha kiliberali (FDP), ambacho ni mshirika mdogo wa serikali ya Kansela Angela Merkel.


Kufuatia matokeo mabaya ya chama chake katika chaguzi za mikoa, Westerwelle amesema kuwa hatogombea tena wadhifa huo, ambao ameushikilia kwa miaka kumi mfululizo.
Kura za FDP zimeshuka hadi 5% tangu chama hicho kilipojiwekea rikodi ya kufikia 14% miaka miwili iliyopita.
Katika siku za karibuni, viongozi wa FDP wa mikoa wamekuwa wakimshutumu waziwazi Westerwelle.
Kamati Tendaji ya FDP inakutana leo, ingawa hadi sasa hakujatajwa mtu makshusi wa kushika nafasi ya uenyekiti.
Westerwelle amekumbana na upinzani mkali baada ya Ujerumani kujizuia kupiga kura kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio la marufuku ya anga dhidi ya Libya. Hatua inaonekana kuitenga Ujerumani na washirika wake, ikiwemo Marekani.
Vile vile, FDP iliukana msimamo wake kuhusu nyuklia baada ya maafa ya Fukushima nchini Japan.

MAN CITY YANYUKA SUNDERLAND 5-0

Manchester City imesogea hadi nafasiya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuitandika Sunderland mabao 5-0.
Yaya
Yaya Toure
City wamewaata kauli wakosoaji kwa kuonesha mchezo maridadi, tofauti na jinsi walivyokuwa wakicheza katika siku za hivi karibuni.
Adam Johnson aliandika bao la kwanza baada ya kupasiana vyema na Yaya Toure.
Carlos Tevez aliandika bao la pili kwa mkwaju wa penati, katika dakika ya 15.
David Silva alipachika bao la tatu, huku la nne likifungwa na Patrick Vieira na Yaya Toure kufunga la tano katika dakika ya 73.
City wameingia katika nafasi ya tatu licha ya kuwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Chelsea.
Mapema, Fulham ilishinda mchezo wake dhidi ya Blackpool.
Mabao mawili ya Bobby Zamora na moja la Dickson Etuhu yaliizamisha Blackpool na kuipeleka katika nafasi ya 11.


  14-year-old Boy Beat His Grandmother Unconscious With a Hammer!


         A 14-year-old boy has been charged as an adult with attempted murder after police said he beat his 66-year-old grandmother with a hammer until she became unconscious.
Hassanhii Garrett has been charged with attempted first-degree and attempted second-degree murder, first- and second-degree assault, reckless endangerment and use of a dangerous weapon, police Detective Kevin Brown said Friday.
       Investigators said the incident happened at about 8:30 a.m. Thursday at a home in the 800 block of East 34th Str

No comments:

Post a Comment