Pages

Pages

Thursday, May 5, 2011

breaking news..!! CHADEMA WAZUA KIMBEMBE TENA!

Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)kimeazimia kufanya maandamano makubwa kutoa elimu kwa Umma kuhusiana mambo kadhaa ambayo chama hicho kinapinga mwenendo wake.
  Wachambuzi wa mambo ya KIsiasa wanasema kuwa moja ya ajenda ambazo wanategemea kusikia nyeti zilizojificha kuhusiana na utajiri wa ridhiwani kikwete ambao haundani na kipato chake toka apate ajira.
   Mikoa ambayo itapitiwa na mikutano hiyo ni Mbeya ,singida,rukwa,morogoro na mji wa sumbawanga kuanzia kesho.




MWILI WA OSAMA KUONYESHWA HADHARANI
Osama laying dead on hospital death bed
Osama Bin Laden Death Photo
   Wasiwasi mkubwa kuhusu ukweli wa mauaji ya mwanzilishi na Kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden, serikali ya nchini hapa inatarajia kutoa picha za mwili wake zilizopigwa kabla ya kuzikwa.
    Tangu Rais Obama atangaze kuuawa na kuzikwa kwa Osama bin Laden, maoni mbalimbali yametolewa yakitaka kuwekwa wazi kwa mwili wake ili ukweli wa tukio zima la mauaji ueleweke duniani.
    Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la CIA, Leon Panetta, alikiambia kituo cha televisheni cha NBC cha nchini hapa kuwa picha ya mwili wake itatolewa ili kumaliza utata huo.
    Kutolewa kwa picha hizo kunatokana na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mvutano mkubwa uliotokea kati ya CIA na maofisa wa serikali juu ya wazo hilo.
    CIA hawakuwa na wazo la kutoa picha kutokana na mwili wake kuwa katika hali ya kutisha, kufuatia kuwa na majeraha makubwa aliyoyapata maeneo ya kifuani na usoni.
Taarifa zilizopatikana awali zilionyesha kuwepo kwa mkanganyiko kuhusu tukio zima la kuuawa kwa Osama huku Ikulu ya Marekani ikishindwa kueleza ni watoto gani wa Osama waliuawa.
     Taarifa nyingine za utata ni maelezo kuwa mke wa Bin Laden aliuawa kwa kupigwa risasi, huku ikiwa haijalezwa wazi kuhusu ulikopelekwa mwili huo.
     Dunia bado imebaki katika kiza kinene kinachohitaji mwanga wa ukweli kutokana na jana maofisa wa nchini hapa kufafanua kwamba mke wa Bin Laden hakuuawa na kusema mwanamke mwingine ndiye aliuawa katika shambulio hilo.
       Maofisa hao walisema mwanamke huyo huenda alikuwa mke wa Sheikh Abu Ahmed, ambaye alikuwa mfanyakazi wa mkewe Osama.
      Ingawa msemaji wa Ikulu, Jay Carney, aliweka wazi kuwa wakati wa shambulio hilo Bin Laden hakuwa na silaha, lakini maofisa walidai Bin Laden alijibu mapigo (alijihami) dhidi ya makomandoo.


WEMA SEPETU ATIWA MBARONI KWA UTOVU WA NIDHAMU






Aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu (27) , mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kutukana hadharani.


Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimtukana matusi ya nguoni msanii wa kizazi kipya, Raheem Rummy 'Rais wa masharobaro' ambapo mshitakikosa lake.


Hata hivyo mshitakiwa huyo alidai mahakamani hapo kuwa aliamua kumtukana mshitakiwa kwa sababu ya dharau zake alizokuwa anamfanyia.


''Mheshimiwa Hakimu si kawaida yangu kutukana ovyo ovyo, lakini hasira zimenifanya nifanye hivyo na ndiyo maana nimekubali kosa langu.


Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, ilidaiwa na Karani Sharifa Dunia kuwa, Aprili 11 mwaka huu Kinondoni, mshitakiwa alimtukana mlalamikaji huyo na kesi imehairishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.
Wema Sepetu katika pozi.


CHRISS BEEZ AKANUSHA KUTAMANI NDOA NA KARRAUCHE TRAN

Chris Brown kuptia mtandao Twitter alizima uvumi uliokua umezagaa kuwa alimuomba mpenzi wake waoane wakati wa sikuu za Easter...
CHRIS BROWN AKIWA NA 'DEM WAKE' KARRAUCHE TRAN
Chis Brown inasemekana kuwa alimuambia dem wake Karrauche Tran kupitia kwenye simu kuwa anamuomba waowane lakini hakuwa na pete kwa wakati huo na mdada huyo kukubali,lakini Chris Brown akafunguka kuwa yeye ni mdogo sana kujihusisha na hizo issue za kuoa kwa sasa coz ndio kwanza ana miaka 21 tu!

No comments:

Post a Comment