Pages

Pages

Friday, May 6, 2011

RAIS MKAPA AJIKABIDHI KORTINI..!!

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa

RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameridhia kupanda kizimbani kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

        Mahalu na mwenzake wanakabiliwa na mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60.
        Wanadaiwa kusababisha hasara hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la ubalozi huo, wakati wa utumishi wao.
       Tayari Rais Mkapa amewasilisha mahakamani hapo hati yake ya kiapo akimtetea Profesa Mahalu na mwenzake kuhusiana na tuhuma hizo zinazowakabili.

      Kwa mujibu wa wakili wa kina Mahalu, Mabere Marando, ikiwa hati hiyo ya kiapo itakubaliwa na upande wa mashtaka na kisha kupokelewa mahakamani basi itatumika kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi bila Mkapa mwenyewe kulazimika kufika mahakamani.

        Lakini kama hati hiyo ya kiapo itakataliwa na upande wa mashtaka, basi Mkapa ameridhia kuwa yuko tayari kufika mahakamani mwenyewe na kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.
Katika hati hiyo ya kiapo, Mkapa amemtetea Profesa Mahalu kuwa amefanya naye kazi kwa muda mrefu na anamjua kuwa ni mtu mwaminifu, mtiifu na mchakapakazi.

       Mkapa alieleza katika hati yake hiyo kuwa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wa uongozi wake na kwamba alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na ununuzi huo na kwamba ulifanyika kwa mujibu wa sheria.

       Alifafanua kuwa mpango wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa ni utekelezaji wa Sera ya Serikali wa kuwa na majengo yake ya kudumu katika kila ubalozi kwa kununua au kujenga ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za upangaji.
Aliongeza kuwa Serikali yake ilimpa Profesa Mahalu mamlaka yote ya kusimamia na kutekeleza mchakato wa ununuzi wa jengo hilo kupitia nguvu ya kisheria aliyopewa na Serikali yake.

        Mkapa alisisitiza kuwa kupitia utaratibu wa Serikali alikuwa akijua kuwa  taarifa ya uthamini wa jengo hilo iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi ilikuwa ni Dola za Marekani 3.0 milioni wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilikadiriwa Euro 5.5 milioni

      “Kupitia utaratibu wa Serikali nilifahamu kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa gharama ya Dola za Marekani 3.0milioni  sawa na Euro 3,098,741.40,” alisema Mkapa na  kuongeza:
“Kupitia utaratibu wa Serikali nilikuwa nafahamu na hivyo kuidhinisha mchakato wote na taratibu za ununuzi wa jengo hilo lililoko Vialle Cortina d’Ampezzo 185 jijini Rome.”

      Mkapa pia alisema kuwa alitambua kuwapo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo na kwamba yeye mwenyewe ndiye aliruhusu kufanyika kwa kuwa ilikuwa ni muhimu katika kutimiza maslahi ya taifa.
Pia Mkapa alisisitiza kuwa alikuwa na bado anatambua taarifa ya serikali bungeni ya Agosti 3, 2004  iliyoeleza na kuthibitisha kuwa taratibu zote za ununuzi wa jengo hilo zilifuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na kwamba dalali alilipwa kikamilifu.



SPIKA MAKINDA AFIWA NA MAMA YAKE 

Mbunge wa Njombe-Kusini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Anne Makinda amefiwa na Mama yake mzazi,Bi Tulikela Samnyuha (86) kilichotokea mkoani Dodoma
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 8 May,2011 Njombe



 BEN KINYAIA NA AUNT EZEKIEL MAHABA MANENE

waigizaji wetu akiponda raha ndani ya bwawa la kuogelea huvu vinywaji laini viburudisha ndimi zao


Kikongwe abakwa akatwa sehemu za siri

        MKAZI wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara, Bi. Mwajuma Selemani (70) amebakwa na watu wasiojilikana na kuchanwa chanwa sehemu za
siri na kitu chenye ncha kali.

     Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoro, Bw. Selemani Farandi amesema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu, wakati bibi huyo akitoka shambani kwake kwenda nyumbani hivyo kukutana na vijana wawili ambao waliamtaka bibi huyo kuwauzia alizeti.


      “Hawa vijana walifika shambani na kumkuta mama akivuna alizeti walimtaka awauzie lakini mama lisema hauzi wakaondoka baada ya muda alirudi mmoja na kumtaka tena auze ndipo mama akapata wasiwasi na kulazimika kuanza safari kurudi njiani,” alisema Asha Iddi mtoto wa mama huyo.


      Alisema akiwa njiani mama huyo alijitokeza kijana ambaye hakufahamika na kumpiga 'ngwara' akaanguka hatimaye kumchania nguo za ndani na kutimiza kumbaka na kumchana chana sehemu za siri na kiti kinachodaiwa kuwa cha ncha kali.


“Pamoja na mama kubakwa kwa mujibu wa Daktari aliyempima ametueleza kuwa aliingiziwa kitu kigumu sehemu za siri kilichomfanya apate maumivu makali amayo kwa sasa yanampa shida hata kujisaidia haja kubwa na ndogo inamwia vigumu,” alisema  Bi. Asha. 
GARI LA TUZO YA TASWA HADHARANI 
      Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na waandishi wa habari wakitazama gari ambalo mwanamichezo bora atapewa kesho katika sherehe za utoaji tuzo walio mahiri katika fani  hiyo. Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inayodhamini tuzo hizo, Teddy Mapunda (wa nne kushoto) alikabidhi gari hilo leo kwa uongozi wa TASWA katika hafla iliyofanyika Hotel ya Movenpick, Dar es Salaam. Kwa Mujibu wa TASWA thamani ya gari hilo ni sh. milioni 13. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo hiyo, Masoud Sanani.


Besigye apofuka macho apelekwaulaya kupata matibabu!!

Dr. Kizza Besigye
                 Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye atapelekwa ng'ambo kwa matibabu zaidi.
Mkewe kiongozi huyo Bi Winnie Byanyima aliambia kuwa madaktari wanaomshughulikia mwanasiasa huo katika hospitali moja Mjini Nairobi wanahofia kuwa Besigye alipata madhara makubwa ya sumu kwenye ngozi na macho yake.
                 Kiongozi huyo wa upinzani alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa na polisi wa Uganda wakati wa kuzima maandamano aliyokuwa akiongoza ya kutembea kwa miguu hadi kazini kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Uganda.
                 Bi Byanyima amemuomba Rais Yoweri Museveni kufanya mashauriano na upinzani pamoja na viongozi wa Kidini ili kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba Uganda badala ya kuwa timua nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano.



 WAANDISHI BORA WAPEWA TUZO

Usiku wa kuamkia leo, katika ukumbi wa Mlimani City, wanahabari bora wa Magazeti, Runinga, Radio, Wapiga Picha na Wachora Katuni walitunukiwa kwa kupewa tunzo na zawadi mbalimbali kwa kuthamini kazi zao nzuri walizofanya mwaka jana. Tunzo hizo za kila mwaka zimeandaliwa na Bararaza la Habari Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na zimepewa jina la Excellence Journalism Awards Tanzania (EJAT). Pichani ni Mweneyekiti Mtendaji wa IPP Media, Bw. Reginald Mengi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi walioshinda sehemu ya tunzo hizo mara baada ya kukabidhi cheti na zawadi.
Mwandishi wa ITV, Festus Sigamonamo (kulia) akipokea tunzo yake kutoka kwa Bi. Fauziat Aboud
Majaji wasataafu wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bi. Blandina Nyoni (kulia)
Bw. Mengi akiwa na Jaji Mstaafu, Mark Bomani
Mtangazaji wa TBC1, Masoud Masoud (kulia) akipokea tunzo yake
Mtangazaji wa Radio Mlimani (Tuma Dandi) kulia, akipokea tunzo yake baada ya kuibuka kidedea
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Bi Joyce Mhaville (kulia) akimkabidhi tunzo mtangazaji Dorcas Raymond wa Channel Ten

No comments:

Post a Comment