Pages

Pages

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEWS...SHEIKH YAHYA AFARIKI DUNIA


Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati,Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia Ijumaa asubuhi jijini Dar es Salaam.
Sheikh Yahya amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco,jijini Dar Es Salaam na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na aliwahi kwenda India kwa matibabu.
Na kwa mujibu wa familia yake,Sheikh Yahya Hussein atazikwa kesho,Jumamosi mchana.....Mungu ailaze roho yake mahali pema....Ameen!!


 
KIPIGO CHASABABISHA LINAH AMKIMBIE AMINI
Linah
Amini 
Linah amesema kuwa hana tena uhusiano na boifriend wake amini ambao wote ni wasanii wa kizazi kipya “Tulikaa tukakubaliana na kila mmoja akaridhia kuwa iwe mwisho wa uhusiano wetu hivyo sababu siwezi kuweka wazi ila mashabiki wangu wajue tumeachana” ailisema linah.
Msanii Amini nae alisema“Dah! bwana ndiyo hivyo kila mtu kwa sasa yupo kivyake ila uelewe sipendi kuzungumzia uhusiano wetu sababu haunisaidii chochote katika muziki wangu.”
wachambuzi wa mambo wanasema kuwa wimbo aliouimba Linah wa Bora Nikimbie ulikua ni kutoka moyoni sababu inadaiwana Amini alikuwa akimpa kipigo Linah mara kwa mara kitendo ambacho alikuwa anakivumilia na kufikia hatua ya kusema bora akimbie


Nato yashambulia meli za kivita za Libya

Mashambulio ya anga kwenye meli za kivita za Libya
Majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato yameshambulia kwa anga meli za kivita nane zinazomilikiwa na jeshi la Kanali Muammar Gaddafi katika uvamizi uliofanywa mjini Tripoli, Al Khums na Sirte.
Katika taarifa iliyotolewa, msemaji alisema Nato lazima ichukue "hatua madhubuti" kuzingatia kuongezeka kwa matumizi ya meli za kijeshi kushambulia raia.
Moto na moshi ulikuwa ukishuhudiwa kutoka kwenye meli zilizoshambuliwa kwenye bandari iliyopo kwenye mji mkuu.
Wakati huo huo, kiongozi wa waasi wa Libya ameomba msaada wa kimataifa kwenye miji iliyo milimani magharibi mwa Tripoli.
Taarifa iliyotolewa na muungano huo wa kijeshi ilisema mashambulio yaliyofanywa siku ya Ijumaa yameonyesha kuwa Nato " ina nia ya kuwalinda raia wa Libya, kwa kutumia nguvu zinazostahili na kwa kiwango kinachofaa."
Naibu kamanda wa Nato nchini Libya, Admeri Russel Harding alisema, "Meli zote zilizolengwa jana usiku zilikuwa za kivita bila kifaa chochote cha raia kushambuliwa."
Haijafahamika kama kuna yeyote aliyeuawa.

 

No comments:

Post a Comment