Pages

Pages

Monday, May 16, 2011

DIAMOND KUWEHUKA BAADA YA KUMWAGWA NA WEMA SEPETU

     Msanii wa kizazi kipya ajulikanae kama Diamond a.k.a The platnum inasemekana amekubwa na msongo wa mawazo kiasi cha kushidwa kufanya mambo yake kama ilivyo ada kutokana na kumwagwa na mrembo Wema sepetu.

      Rafiki wa karibu wa msanii huyo waliwahi kumuonya achane mapema na demu huyo kwani yupo kimaslahi zaidi ila yeye alilemaza shingo na kudhani kuwa alikuwa akipendwa kwa dhati na kisio lake la kumuoa Wema litatimia kumbe ndo analisogelea jumba bovu.


MARY JOEL VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTER 2011

Mwanadada Mary Joel (katikati) amenyakua taji la kuwa Vodacom Miss Arusha City Center 2011 katika ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini. Pembeni yake kulia ni mshindi pili Neema Edward pamoja na Stacey Alfred. Shindano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Triple A, Arusha.
Mwanadada Zahra Seleman ambaye ni Vodacom Miss Arusha City Center 2010 akimvalisha taji Mary Joel ambaye amekuwa Vodacom Miss Arusha City Center 2011. Shindano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Triple A, Arusha.


Mkuu wa IMF azuiliwa korokoroni New York

Dominique Strauss-Kahn
Mkuu wa Shirika la IMF Dominique Strauss-Kahn
Mkuu wa Shirika la fedha duniani ( IMF ) ,Dominique Strauss-Kahn, amezuiliwa katika gereza moja la wafungwa sugu ya Rikers Islands mjini New York, kwa tuhuma za kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli.
Jaji amesema kulikuwa na tisho la Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, kutoroka iwapo angeachiliwa kwa dhamana. Mkurugenzi huyo alikamatwa jumamosi iliopita punde baada ya kuabiri ndege. Baadaye alishtakiwa kwa kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja mjini New York.
Strauss-Kahn anakabiliwa na mashtaka saba na huenda akapewa kifungo cha hadi miaka 25 jela ikiwa atapatikana na hatia.
Mkuu huyo wa shirika la IMF amekanusha mashtaka dhidi yake.
Mawakili wake wameelezea kukasirishwa kwao baada ya kunyimwa dhamana , lakini wakasema mteja wao hatimaye ataondolewa lawama.
''Makabiliano ndiyo yameanza'', wakili wa upande wa utetezi Benjamin Brafman aliiambia mahakama.
Kutokana na kuzuiliwa kwake, Strauss-Kahn alishindwa kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka umoja wa ulaya mjini Brussels, Ubelgiji ambako mkopo wa kunusuru uchumi wa Ureno, wa kiwango cha dola milioni mia moja na kumi uliidhinishwa.
Nchi ya Ureno imekuwa ya tatu inayotumia sarafu ya Euro kupokea msaada kutoka kwa umoja wa ulaya na shirika la IMF, baada ya Ugiriki na Ireland.

RIHANNA AJIPEREKA KWA CHRIS BROWN?!


RIHANNA
Rihanna ameanza kujigonga kwa mpenzi wake wa zamaniChris Brown baada ya juzi Ijumaa kumfata kwenye mtandao wa Twitter na Chris Brown naye kumjibu faster....

CHRIS BROWN
RiRi alikua hawasiliani na Chris Brown kwa miaka 2 sasa tangu mwaka 2009, na ni ajabu kwa kumpata coz yeye ana twitter followers kama milioni 5 hivi na baadaye Rihanna akajishitukia na kutupia kwenye twitter kuwa watu wasije wakafikiria vingine coz ni twitter tu na kwa sasa Chris Brown amemaliza tour yake ya nchini Australia na kwa sasa ana-shoot video mpya na Justin bieber iitwayo Next to You jijini Los Angeles


No comments:

Post a Comment