Pages

Pages

Sunday, May 15, 2011

Dkt SLAA AMCHANA NAPE..!!!!

                                                                                 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha vikali tuhuma kuwa Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe ameagiza
chama kununua magari yake matatu aina ya Fuso, kufafanua kuhusu mshahara wa Katibu Mkuu wake, Dkt.    Willibrod Slaa na kuibua tuhuma mpya dhidi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye.
         Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA, Bw. Antony Komu alisema tuhuma hizo zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye zinalenga kuwachafua viongozi wa chama hicho na kupotosha ukweli juu ya vita inayopiganwa na CHADEMA dhidi ya ufisadi na mafisadi.
"           Madai kuwa Dkt. Slaa ameshinikiza kulipwa sh. mil. 7.5 siyo kweli, tunaomba ieleweke kuwa hajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka kuaminisha umma," alisema Bw. Komu.
          Akiwa na maofisa wengine wa CHADEMA, Bw. Mabere Marando na Profesa Abdallah Safari, Bw. Komu alisema Dkt. Slaa analipwa sh. mil.7.1 ambazo zimejumuisha mshahara na marupurupu yote.
         "Dkt. Slaa analipwa posho yake binafsi ambayo inaweza kuitwa mshahara sh. 1,725,000 wakati mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi, Katibu wa CHADEMA analipwa mafuta ya kuja ofisini na kurudi nyumbani lita 30 kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi, bei ya kila lita moja sh. 2,000" alisema Bw. Komu.
          Alisema wakati Dkt. Slaa analipwa kiwango hicho mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi kwa bei ya kila lita moja sh. 2,500 bei ambayo haipo lakini bunge linaridhia kulipa.
        Bw. Komu anaendelea kusema kuwa ingekuwa sahihi kusema kuwa Dkt. Slaa ananufaika sawa na mbunge kama angekuwa analipwa zaidi mbali ya sh. mil. 7,174,000 anazogharimiwa na chama.
"Mbunge akikaa katika kikao cha Kamati ya Bunge au akihudhuria mkutano wa bunge analipwa posho ya sh. 70,000; sh. 30,000 posho ya mafuta na sh. 80,000 posho ya kujikimu akiwa Dodoma, fedha hizi zinalipwa bila kujali kama mbunge huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na amekwenda nalo Dodoma," alisema Bw. Komu.
       Alisema mbunge anapewa mkopo wa sh. mil. 90 ambazo anatakiwa kulipa nusu ya fedha hizo, mzigo unaobaki unabebwa na serikali na pia serikali hiyo hiyo inamdhamini kukopa sh. mil. 200 kutoka vyombo vya fedha.


TP Mazembe yatolewa, Simba kusonga mbele

Mabingwa watetetezi wa Klabu Bingwa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Mazembe
TP Mazembe
    Shirikisho la Soka barani Afrika Caf limechukua hatua hiyo kufatia malalamiko ya Simba ya Tanzania kuhusu kuchezeshwa kwa Janvier Besala Bokungu.
    Mazembe iliichapa Simba 6-3 katika mechi mbili walizocheza.
Simba sasa itapambana na Wydad Casablanca ya Morocco, ambayo ilifungwa na Mazembe katika raundi ya tatu, kupata nafasi ya katika ngazi ya makundi.
Simba na Wydad casablanca watakutana katika uwanja utakaotangazwa wiki ijayo.
    Mazembe imeshinda ligi ya mabingwa Afrika kwa miaka miwili iliyopita, na kufika fainali ya klabu bingwa ya Dunia mwaka jana, na kutolewa na Inter Milan ya Italia kwa mabao 3-0.
 

No comments:

Post a Comment