Pages

Pages

Wednesday, May 11, 2011

DAWA ZA KULEVYA ZAMFIKISHA PABAYA FEROUS WA DAZ NUNDAZ

          Msanii wa kizazi kipya ferouz toka kundi la Daz nundaz amekanusha skendo ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo wachambuzi wa mambo ya kitaani walidai kwamba jamaa anatumia mihadarati kupita kiasi kitu ambacho kimempelekea kushuka kimuziki na kimapato pia.

        Ferous aliibuka na kudai kuwa ni maneno ya watu na maneno hayo hayana ukweli wowote kwani mtu atumiae mihadarati "TEJA"awezi kumiliki usafiri kama anavyomiliki yeye.
       Swali la wazi kwa mchizi ni kwamba je unadhani mateja wote hawana fedha na uwezo wa kumiliki magari ya kifahari? wapo matajiri na mawaziri wanatumia hiko kitu.
       Mchizi aliwahi kutamba na songi kali kama vile kamanda,Barua na maji ya shingo enzi za ujana wa mwanabongo freva huyo.






CHRISS BROWN AJIMWAGA KIMALAIDAVI CLUB SIKU YAKE YA KUZALIWA
          Chriss Beez amefanya bonge la party katika club moja huko Las vegas iitwayo Vegas hotspot pure night club ikiwa ni sherehe ya kutimza miaka 22 tangu azliwe.
         Bizz alikuwa macho muda wote juu ya mpenzi wake Karruache  maana alionekana mida mingi kula denda na mahug ya muda mrefu na kidosho ingawa klikuwa na jimama flani ambalo lilikuwa linamganda sana Bizz aondoke nalo lakini mwisho wa party alisepa kiaina na mwanamitindo huyo ampendae sana kwa sasa.





         MAWAZIRI VICHECHE WANYOSHEWA KIDOLE NA JK
            KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana alimshtaki Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa wapiga kura wake, akiwaeleza kuwa kiongozi huyo na Rais Jakaya Kikwete wanazidi kuongeza umaskini wa taifa kwa kufuja fedha za walipa kodi kwa matanuzi mbalimbali ikiwemo kufanya semina elekezi za gharama kubwa na zisizo na tija.
            Dk. Slaa alitoa tuhuma hizo wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa vijiji vya Majimoto, Mbede na Usevya vilivyoko katika jimbo la Katavi linaloongozwa na Waziri Mkuu huyo, katika mfululizo wa maandamano na mikutano ya chama hicho inayoendelea katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
            Katika hotuba zake zilizoonekana kuteka hisia za wakazi wa jimbo hilo ambao walikuwa wakimshangilia mara kwa mara, Dk. Slaa alisema inasikitisha kuona Pinda akifurahia anasa za uwaziri mkuu, kama kufanya semina elekezi za gharama kubwa na kutembelea gari alilodai lina thamani ya sh milioni 500, huku wapiga kura wake wakiwa na hali ngumu ya maisha.
             Akilinganisha kile alichokiita “matanuzi ya Pinda na Kikwete” na hali halisi ya maisha ya watu wa jimbo hilo na maeneo mengine ya mkoa wa Rukwa na Katavi, Dk. Slaa alisema si haki kwa wananchi hao kuendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na nyasi wakati kodi zikifujwa kila kukicha.
            Akitoa mfano wa jinsi kodi za wananchi zinavyofujwa, Dk. Slaa alisema semina elekezi kwa mawaziri inayoendelea mjini Dodoma imegharimu fedha nyingi ambazo zingetosha kabisa kujenga shule za sekondari katika jimbo zima la Pinda bila wananchi kuchangisha hata shilingi moja.
           “Leo Pinda na Kikwete wamekutana pale Dodoma kwenye semina elekezi. Posho ya siku tatu wanayoitafuna pale Dodoma ingetosha kabisa kujenga shule za sekondari bila ninyi kuchangishwa hata shilingi. Kule wapo mawaziri wote 50 na kila mmoja kwa siku analipwa posho ya sh 200,000 sasa piga hesabu mwenyewe kwa wiki nzima na kwa watu wote 50 watakuwa wametafuna kodi yako kwa kiasi gani? Ongeza na mafuta wanayotumia kwenye magari yao kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa bei ya lita moja ya petroli ya zaidi ya sh 2,000 halafu uone jinsi wasivyo na huruma na ninyi.
            “Watu wake hamna nyumba bora, hamna chakula cha kutosha, hamna zahanati wala shule bora, halafu Pinda wenu na Kikwete wanakwenda kufanya matanuzi kwenye semina elekezi Dodoma. Semina zenyewe hazina tija. Kikwete amewateua mwenyewe mawaziri halafu anawaandalia semina za kazi gani? Kama aliona hawana uwezo wa kuongoza si angeteua wengine?” alisema.

               Alisema wakati Pinda anatembelea gari la milioni 500 na kusaini posho ya sh 200,000 bungeni, wananchi wengi wa jimbo lake bado wanaishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi wakati kwa nafasi yake kama waziri mkuu angeweza kuisadia serikali kubana matumizi na kuokoa fedha za kugharamia miradi ya maendeleo ya wananchi
              “Gharama ya gari analotembelea Pinda, mbunge wenu ni sawa na kujenga vituo vya afya vitano…maana kila kituo kimoja cha afya ni sh milioni 100. Wakati Pinda anatembelea gari hilo, hapa Majimoto hamna kituo cha afya hata kimoja!” alishangaa na kusisitiza Dk. Slaa na kuongeza: “Tena Pinda huwa anatembea na msafara wa magari 30 ya wasaidizi wake na kila moja ni sh milioni 200 kwa hiyo anatembea na jumla ya sh bilioni 600!
                 Bilioni 600 ndugu zangu ni sawa na vituo vya afya 60, jimbo lenu lina kata 22 tu kwa hiyo pesa hiyo ingeweza kuwapa vituo vya afya mara mbili zaidi. Zinaweza kujenga shule za sekondari, vituo vya afya katika kila kijiji hapa kwenu, zinaweza kuwasaidia kuwa na nyumba za bati …zinaweza kubadilisha maisha yenu. Lakini Pinda anatembea nazo barabarani…inauma sana ndugu zangu,” alisema.
                Alisema inasikitisha zaidi kuona Pinda anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua katika nyumba yake iliyoko jimboni badala ya kupeleka umeme ambao ungeweza kutumiwa na wananchi wote.
               “Ndugu zangu ninakerwa sana ninapoona waziri mkuu anakuwa mbinafsi, pale kwenye ile nyumba yake amejiwekea mwenyewe umeme wa jua (solar) wakati ninyi wapiga kura wake mkiwa kwenye giza….huu ni ukatili mkubwa sana.
             “Waziri Mkuu anashindwa kushughulikia matatizo ya wafugaji jimboni kwake, ng’ombe wa watu wake wanapigwa risasi na watu wake mnapigwa risasi yeye hafanyi lolote. Nimetoka katika kijiji cha Majimoto kule wenzenu wanakunywa maji ya sumu….waziri mkuu ambaye ni mbunge wenu kwa zaidi ya miaka 10 anaacha mfe kwa maji ya sumu wakati yeye akibaki salama. Bungeni akiulizwa anasema maji hayo yamepelekwa kwa mkemia mkuu Dar es Salaam…Dar es Salaam na Usevya ni mbingu na ardhi. Watu wanazidi kuathirika kwa sumu…inanitia uchungu sana,” alisema.
              Aliweka wazi kuwa kazi yake na ya chama chake ni kujenga chuki ili wananchi wamchukie kiongozi na serikali yote ambayo haitimizi mahitaji yao licha ya kukusanya kodi ya sh bilioni 420 kwa mwezi kutoka kwao.
             Alisema hali ya maisha imezidi kuwa ngumu kwa sababu ya serikali ya kifisadi na sera mbovu za CCM ambayo pamoja na mambo mengine imeweka kodi kubwa hata kwenye bidhaa na huduma za msingi zinazogusa maisha ya watu.
              Akitoa mfano alisema wakati mfuko mmoja wa saruji unauzwa kwa sh 20,000 ndani ya jimbo hilo, takwimu za kodi kutoka katika kiw anda cha Twiga Cement za hadi kufikia Oktoba mwaka jana zilionyesha kuwa mfuko mmoja wa saruji unatozwa kodi ya sh 7,500.

            Alisema kama kodi hiyo ingeondolewa au kupunguzwa wananchi wengi wa jimbo hilo na Watanzania wote kwa ujumla wangepata unafuu na kuwa na uwezo wa kujenga nyumba bora za kuishi.
           Akigusia kauli ya Rais Kikwete ya kuwataka mawaziri wazinzi na wasiofanya kazi wajiondoe wenyewe Dk. Slaa alisema kauli hiyo inazidi kuonyesha jinsi Kikwete alivyo kiongozi dhaifu na asiyeweza kuchukua hatua hata pale anapoona kuna tatizo.
           “Leo anasema mawaziri walioshindwa kazi na wanzinzi wajiondoe wenyewe. Maana yake ni kwamba anajua mawaziri wake hawafai lakini badala ya kuwatimua anawapa ruksa wajiondoe wenyewe….lakini simshangai, hiyo ndiyo kawaida yake. Aliwahi kuwaambia wanaotumia madawa ya kulevya waache wenyewe leo watumiaji wa madawa ya kulevya na wauza unga wanaendelea. Fedha zenu za EPA zilipoibiwa kule benki kuu, Kikwete aliwaambia wale wezi wazirudishe wenyewe badala ya kuwakamata. Na aliwahi kuwapa wala rushwa muda ili waache wenyewe leo rushwa inazidi kukithiri….simshangai,” alisema Dk. Slaa.
            Katika mikutano hiyo maelfu ya wananchi yalionekana yakirudisha kadi za CCM na kupokea zile za CHADEMA ingawa idadi kamili haikuweza kupatikana mara moja.
                Dk. Slaa aliyeambatana na kada mwandamizi wa chama hicho, Fred Mpendazoe, aliwataka wakazi wa jimbo hilo kuzidi kuiunga mkono CHADEMA kwani imedhamiria kuwakomboa Watanzania kwa kuchukua dola mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment