Pages

Pages

Wednesday, May 11, 2011

MAJASUSI YA KIMAREKANI YAMSAKA MULA OMAR



    MULA OMAR,gaidi mkubwa duniani anaesakwa na majasusi ya U.S.A

     VIKOSI maalumu vya Marekani na Pakistani, vimeanza harakati za kumsaka kiongozi wa wanamgambo wa Taliban,Mullah Omar, baada ya kupata taarifa mpya kuhusu mahali alipo kiongozi huyo.Taarifa za kiupelelezi zinadai kuwa, kiongozi huyo mwenye jicho moja, anadaiwa kuwa amejificha katika mji uliopo Magharibi mwa Pakistani, Quetta, karibu na mpaka wa Afghanistan.

      Mtandao wa makachero wa Pakistan (ISI), unasema kuwa, kikosi hicho kimepania kumkamata kikiwa cha kwanza baada ya kusononeshwa na oparesheni ya Marekani, ambayo ilisababisha kifo cha kiongozi wa Al Qaeda, Osama Bin Laden.

       Imeelezwa kuwa, timu hiyo ya kikosi cha Marekani imeamua kuanzisha msako dhidi ya Omar, baada ya kukusanya taarifa nyingi kutoka nyumbani kwa Bin Laden, katika mji wa Abbottabad.

     Mbali na Mullah, kikosi hicho cha Marekani kinataka kuwahoji wake watatu wa Bin Laden ambao wanashikiliwa nchini Pakistan waliokutwa naye wakati akiuawa.

      Hata hivyo, Omar(52), ambaye alikuwa akimlinda Bin Laden nchini Afghanistan, wakati wa shambulizi la Septemba 11,2001, anasemekana kuwa, amezungukwa na mamia ya wapiganaji wenye silaha na inatarajiwa watakuwa wakifuatilia kuhusu kushambuliwa.

       Mmoja wa makachero waandamizi kutoka ISI ambaye alithibitisha kuanza msako wa kumsaka Mullah, amesema kuwa: "Kuna hatua kubwa za kijeshi zitakazochukuliwa hivi karibuni katika mji wa Quetta.

    "Uamuzi huo umechukuliwa kabla ya Marekani kupata nafasi ya kurudia mpango iliyoufanya dhidi ya Bin Laden. Tujaribu kumpata akiwa hai, lakini endapo ataleta upinzani, tutamuua," amesema ofisa huyo.

     Omar ambaye alikuwa mtu wa karibu na mlinzi mkuu wa Osama nchini Afghanistan wakati wa shambulizi la Septemba 11,2001, pia ametangaziwa dau la dola milioni 25, endapo utapata kichwa chake.

     Mchakato huo pia ni wa kumsaka naibu kiongozi wa al-Qaeda, Ayman Al-Zawahiri, ambaye anasemekana kuwa, yupo Pakistan.



WILAYA YA KYELA YAKUMBWA NA MAFURIKO
Wilaya ya Kyela imekumbwa na mafuriko, ni kuanzia eneo la Tenende kuelekea Ipinda. Barabara pamoja na vijiji vilivyoko kwenye maeneo hayo vilikuwa vimefunikwa na maji hadi jana jioni
 Eneo la Tenende huko Kyella, inaelezwa kuwa mafuriko hayo yanatokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Rungwe tangu juzi.



MISS MWANZA KUZINDULIWA KWA MBWEMBWE
              UZINDUZI wa shindano la urembo kumsaka Miss Mwanza 2011, unatarajiwa kufanyika
Juni Mosi, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Crest iliyopo
katika jengo la PPF, katikati ya Jiji la Mwanza.
            Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, waandaaji wa shindano
hilo, John Dotto, uzinduzi huo utaambatana na utambulisho wa warembo
watakaochuana katika kinyang’anyiro hicho.
            Alisema kuwa tayari warembo wameshaanza kujiandikisha kuwania Umalkia wa Mwanza
na kwamba wanaojiona kuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo, wanakaribishwa
ambapo fomu zinapatikana katika ofisi za hoteli hiyo.
          “Bado tunakaribisha warembo wenye sifa kujiandikisha kwa sasa kwani baada ya
uzinduzi, hatutapokea mrembo yeyote yule, hata awe na sifa kiasi gani,” alisema.
Alisema kuwa shindano lao linatarajiwa kuwa la kiwango cha juu, kuanzia
maandalizi yake, warembo na shoo ya kilele cha kinyang’anyiro hicho.



Watu 80 wauawa Sudan Kusini

Wanjeshi wa SPLA
Wanjeshi wa SPLA
                Watu wasiopungua themanini wameuawa katika eneo la Sudan kusini baada ya waasi kuvamia kambi za mifugo, jeshi la Sudan kusini limesema.
                Wavamizi hao waliwauwa watu 34 wakiwemo wanawake na watoto, wakati walipoiba mifugo katika jimbo la Warrap, amesema msemaji wa jeshi Philip Aguer.
              Lakini wakati wakitoweka na mifugo, wezi hao walishambuliwa na 48 kati yao kuuwawa.
Sudan kusini inajitenga na eneo la kaskazini mwezi Julai mwaka huu. Sudan Kusini inaishutumu Khartoum kwa kusababisha hali ya wasiwasi katika eneo hilo.
Rais wa Sudan
Rais wa Sudan
             Madai kama hayo yamepingwa na serikali ya Rais Omar al-Bashir.
Umoja wa mataifa umesema kuwa makundi yasiyopungua saba ya wapiganaji waliojihami yanaendesha shughuli zake Sudan Kusini.
           Umoja wa mataifa unakadiria kwamba zaidi ya watu 1,000 wameuawa mwaka huu katika mapigano kati ya waasi au makundi yaliyojihami na jeshi la Sudan Kusini.
Jamii nyingi za eneo la Sudan Kusini pamoja na mataifa jirani hutegemea sana mifugo kwa maisha yao.

No comments:

Post a Comment