Pages

Pages

Tuesday, May 3, 2011

RIDHIWANI AUKANA UBILIONEA...DR SLAA KUJIBU MAPIGO?

            MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Ridhiwan Kikwete, amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake juu ya kumiliki mali na mabilioni ya fedha.
Ridhiwan alikanusha madai hayo baada ya nyakati tofauti Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mchungaji Christopher Mtikila kutoa madai kuwa Ridhiwan pamoja na kumaliza shule miaka michache iliyopita, hivi sasa ni tajiri bilionea.
          Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Ridhiwan, alisema habari hizo si za kweli bali za kizushi na kwamba zimejaa uongo unaolenga kumchafua yeye pamoja na baba yake Rais Jakaya Kikwete huku wakipandikiza chuki kwa umma.
         Ridhiwan alisema kwa sasa anamiliki shamba la hekari moja na nusu, gari aina ya Toyota Cami na akaunti tatu tofauti zilizo katika benki ya NBC, Stanbic na CRDB.
        Alipoulizwa mbona anaonekana akitembelea magari ya kifahari, mtoto huyo wa Rais alisema: “Hapa mjini unaweza kumuona mtu amevaa suti ukadhani ya kwake kumbe ameazima. Mimi nina marafiki wengi, huwa wananiazima magari yao nitembelee, juzijuzi hapa nilikuwa na benzi ya rafiki yangu….jamani miundombinu ya mjini si mnaijua?”
        Alisema kutokana na kuwaheshimu wazee hao na umri walionao ni bora watumie busara na kujitokeza ili watoe ushahidi juu ya hayo waliyoyasema na hatua zaidi zichukuliwe.
Aliongeza kuwa iwapo itadhihirika kuwa habari walizozieleza ni za uongo basi atakuwa tayari kuwasamehe; lakini alidai leo atawafikishia barua wazee hao ambapo ndani ya wiki mbili amewataka wathibitishe taarifa hizo walizozitoa juu yake.
        “Kama haitoshi narudia tena niliwaahidi ushirikiano na endapo watataka ili kuthibitisha yote hayo waliyosema na hata yale wanayoyasikia, wakithibitisha habari walizopewa ni za uongo basi wasisite kuueleza umma,” alisema Ridhiwan.


STL ATIMBA UJERUMANI NI KWAJILI YA NUSU FAINALI

            Yule  Rapper wa kike aliweka maskani yake nchini Norway,Stella Mwangi aka STL toka kenya amewasili nchini Ujerumani kwenye nusu fainali za Euro Vision iyakayofanyika mjini Dusseldorf tarehe 10 May2011
STL anaiwakilisha Norway na anatarajiwa ku-perform track yake kali ya Haba Haba na atashindana na artist toka Albania,Finland,Georgia,Russia,Serbia, Switzerland,Armenia,Poland na Uturuki na kama akipita ataingia fainali itakayofanyika May 12,2011
STL ana track kali kama Take It Back na Biashara na nyimbo hizo zimetumika kama soundtracks kwenye movie za American Pie,Save the Last Dance naCSI New York

WATU 300 WAZAMA KWENYE MAJI DRC

Mitumbwi nchini DRC
            Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kufa baada ya chombo walimokuwa ndani kuzama katika Ziwa Kivu, kusini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
           Mwandishi watu, amesema ajali hiyo ilitokea katika mji wa Tshikapa, Kusini mwa DRC. Ajali hiyo ilitokea jumapili usiku.
          Mashua hiyo ya kusafirisha mizingo inasemekana ilizama ikiwa na zaidi ya watu 300.
          Maafisa wanasema idadi kamali ya watu waliofariki haijulikana. Hata hivyo watu 30 wanasemekama wamenusurika baada ya kuogelea hadi kwa ufukwe wa ziwa hilo.
         Ajali ya sasa imetokea wiki moja baada ya watu 50 kufa katika ziwa hilo upande wa Mashariki, pale mtumbwi wao ulipozama. Shughuli za uokozi zinaendelea.



Wow, this chick has to be in the running for being one of the baddest in the game right now.  Just look at those abs!  Jordin Sparks is killin em’ right now and we’re not made she’s sharing this picture.

No comments:

Post a Comment