Pages
▼
Pages
▼
Tuesday, May 10, 2011
SUGU AMPASUA JANUARI MAKAMBA
Mbunge wa mbeya mjini(CHADEMA) Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU amemchana mtoto wa makamba ajulikanae kama Januari Makamba katika mkutano wa maandamano ya amani uilofanyika jana mjini Sumbawanga ambapo umati wa watu maelfu ya watu ulikusanyika kusikiliza elimu kwa umma toka kwa viongozi wa CHADEMA.
Aidha Dr. Slaa nae aliibuka na kusema kwamba ameibamba nyaraka moja ya CCM ambayo inaonyesha kuwa CCM wamekili kuzidiwa nguvu na vyama vingine mpaka kupelekea kujivua gamba kutokana na kupoteza mvuto kwa wananchi kama ilivyokuwa wali.
Pia Sugu alimtolea uvivu Ridhiwani kikwete na kudai kuwa nae ni mmoja wao kati ya watu wanaowaandama kutokana na mali walizojipatia kiharakaharaka ambapo Dr. slaa ameahidi kumburuza kortini kijana huyo ambaye baba yake ni Rais wa jamhuri ya mungano wa TanzaniaK
Kwa upande wa sugu anahasira sana na vijana hawa ukizingatia toka aingizwe town katika ule mradi wa maralia ni vita kwa kwenda mbele.
LIVERPOOL YAIFANYA KITU MBAYA FULHAM
Liverpool imejiongezea matumaini ya kumaliza katika timu nne za juu baada ya kuiangushia kisago cha mabao 5-2 Fulham kwenye uwanja wa Craven Cottage.
Rodriguez amefunga magoli sita katika mechi mbili
Maxi Rodriguez alifunga mabao matatu peke yake, huku akifunga goli la kwanza katika sekunde ya 32.
Maxi alifunga goli la pili katika dakika ya saba, na lake la tatu katika dakika ya 70. Dirk Kuyt na Luis Suarez walifunga magoli mengine ya Liverpool.
Moussa Dembele na Steve Sidwell walifunga magoli mawili ya Fulham, ambao walikuwa wakicheza nyumbani
No comments:
Post a Comment