Pages

Pages

Wednesday, June 8, 2011

MGANDA AFANYA BIASHARA NA ELTON JOHN


 

Afrika Mashariki yakabliwa na Njaa


 Msanii toka Uganda anayeishi Uingereza,Tazz Mujagata ni mmoja kati ya wasanii wanaokuja juu sana,coz amepata offer toka kwa Sir Elton John baada ya kuvutiwa na live perfomance zake pamoja na mashairi yake mazuri na kumfanya Sir Elton John moja ya track zake

Ngoma yake iitwayo Remember,imetesa sana barani Ulaya tangu itue kitaa na ya Mpapula ilifanikiwa kushinda tuzo ya ECO media kama Best song & Video award 2011

SIR ELTON HERCULES JOHN
Kwa sasa anatarajia kutia maguu Kampala kwa ajili ya kuandaa album launch yake mwakani na inasemekana kuwa anapiga sana show na ana booking ya miezi 6 ijayo kupiga show Europe na wengi wanamtabiria kuwa ni Dr Jose Chameleon mpya na tracks zake zinapatikana kwenye Facebook, Youtube na Myspace na ngoma zake za Reggeaton,Ragga na RnB zitasambaa nchini Uganda hivi karibuni na ni mmoja wa artist aliyepata shavu la ku-perform kwenye Uganda Independence day cerebrations nchini Uingereza na Marekani

Njaa
                Shirika moja la kimarekani limeonya kuwa janga kuu la uhaba wa chakula duniani linaendelea kubana mashariki mwa upembe wa Afrika.
        Uhaba wa chakula waathiri Afrika Mashariki

Shirika hilo lijulikanalo kama The Famine Early Warning Systems Network limeonya kuwa nchi zinazotia wasiwasi ni Ethiopia, Kenya na Somalia.
      Limesema usaidizi mkubwa wa dharura unahitajika kuokoa maisha na kukabiliana na utapiamlo katika eneo hilo.
Shirika hilo pia limesisitiza kuwa usaidizi unaotolewa kwa sasa hautoshi.
        Katika taarifa yake shirika hilo limesema kuwa eneo la upembe wa afrika limeathiriwa na upungufu wa mvua kwa misimu miwili hivyo kusababisha ukame mbaya zaidi tangu mwaka 1995

No comments:

Post a Comment