Pages

Pages

Friday, September 16, 2011

MKENYA AINGIA UWANJANI AKIWA UCHI WA MNYAMA


Jamaa mmoja mwenye asili ya kenya aliingia uwanjani akiwa uchi wa mnyama kwenye mechi kati ya England na Argentina kwenye michuano ya Rugby World Cup - 2011 inayofanyika nchini New Zealand .

Inasemekana jamaa ni mzaliwa wa Kenya ana miaka 23 na alikua hajavaa kitu zaidi ya kuchora uso wake,na alikatiza kwenye uwanja wa Otago na kuonekana na mamilioni ya watazamaji wa television duniani,baadaye alikamatwa na wana usalama na huenda akakabiliwa na kifungo che miezi 3 jela au faini ya dola 5,000.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa jamaa huyo aliamua kufanya hivyo ili kujizolea umaaru duniani.


SOKO LA MBEYA LATEKETEA LEO



ASUBUHI YA LEO TAREHE 16.09.2011 NCHI IMEINGIA KATIKA JANGA LENGINE AMBAPO SOKO KUU JIPYA LA SIDO MWANJELWA MKOANI MBEYA LILITEKETEA KWA MOTO MAJIRA YA SAA 9:50AM ASUBUHI, MOTO HUO AMBAO ULISIMAMA UKIWAKA KWA MUDA WA MASAA MAWILI BILA KUZIMIKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA KUPOTEZA MALI ZA WATU WENGI. IKIWA NI MIAKA MICHACHE TUU  KUPITA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUPATA PIGO KUBWA BAADA YA SOKO KUU LA MWANJELWA KUUNGUA MOTO NA KUWALAZIMU WAANZE UPYA BIASHARA ZAO.

No comments:

Post a Comment