Pages

Pages

Thursday, September 15, 2011

USAIN BOLT AVUNJA REKODI YA DUNIA ALIYOIWEKA


 Kutota huko Zagreb, Croatia: Usain Bolt amefanikiwa kuvunja rekodi yake aliyoiweka kwenye mbio za mita 100 tangu alipowekwa kando kwenye michuano ya dunia iliyopita mara baada ya kukosa sifa na safari hii akishinda kwa kutumia sekunde 9.85 kwenye michuano ya dunia iliyofanyika jana mjini Zagreb.

MGONJWA ANATAFUTA NDUGU ZAKE, YUPO (ICU) HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Picha ya mgonjwa anayetafuta ndugu zake akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili ilipokea mgonjwa toka Hospitali ya Mwananyamala tarehe 18/08/2011 akiwa mahututi na hajitambui.

Inasemekana kuwa mgonjwa huyu aliokotwa na wasamaria wema barabarani akiwa amegongwa na gari usiku wa kuamkia tarehe 18/08/2011 ambao walimpeleka katika hospitali ya Mwananyamala.
Kkutokana na maumivu aliyokuwa nayo kwa muda huo, hospitali ya Mwananyalama iliamua kumpleka katika hosp[itali ya Taifa ya Muhimbili ili aweze kupata huduma na uchunguzi zaidi.
Mgonjwa huyo hajulikani jina lake wala anakotokea kutokana na kutoongea toka alipookotwa na kufikishwa katika hospitali ya Mwananyamala siku hiyo ya kwanza.
Baada ya kufikishwa Mhimbili mgonjwa huyo alifanikiwa kuangaliwa na madaktari bingwa siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 na kufanyiwa uchuguzi wa vipimo mbalimbali ikiwemo X-Ray ya tumbo, kichwa, kifua na kiuno.
Majibu ya vipimo hivyo yalionyesha kuwa kulikuwa na damu kidogo iliyoganda kichwani kutokana na kuvujia kwa ndani. Picha za kifua na kiuno zilionyesha kuwa hakuna tatizo, huku picha ya tumbo ilionyesha kuwa bandama ikikuwa imepasuka hali iliyopelekea kufanyiwa upasuaji siku hiyohiyo ili kuiondoa bandama.
Baada ya upasuaji huo kukamilika mgonjwa alipelekwa moja kwa moja hadi chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) siku hiyo hiyo.
Tangu apelekwe ICU hali yake bado ni mbaya kwani bado, hajitambui.
Natangu siku hiyo hadi leo hii hakuna ndugu au jamaa yoyote aliyejitokeza kuulizia hali ya mgonjwa huyu.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili unaomba yeyote anayemfahamu mgonjwa huyu atoe taarifa kwa ndugu na jamaa zake ili waweze kuja kumtambua.
Kwani hospitali hiyo inaendelea kumpa huduma zote ikiwemo chakula na malazi bila tatizo lolote.

No comments:

Post a Comment