Pages

Pages

Monday, October 3, 2011

CABO SNOOP ATUA DAR KUFANYA ONYESHO


    
Msanii mahiri kutoka nchini Angola,ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake kadhaa hapa nchini,ikiwemo wimbo wa Prakatatumba na Windeck,baada ya kulitikisha jiji la Nairobi kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011 lililofanyika jana,jioni ya leo ametua jijini Dar kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere akiwa ameambatana na Crew yake,msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza Oktoba 9, ambayo itakuwa  ni siku ya kifamilia a.k.a Family Day kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.Pichani mlangoni shoto ni Cabo Snoop akiwa ameambatana na mwenyeji wake kutoka Kampuni ya Prime Time Promotion,Balozi Kindamba,mbele kabisa ni Meneja wa msanii huyo .


CHADEMA YASUSIA MATOKEO IGUNGA,CUF YAANGUKIA PUA
   Chama chadema kimegomea matokeo ya ubunge jimbo la Igunga ambapo wanadai kuna vitu ambavyo havijaenda sawa,hivyo kimekimejipanga kufanya mapinduzi ya kidemokrasia na muda si mrefu wataongea na vyombo vya habari.
   Kongozi wa  chama hiko amesema CHADEMA hakijasaini kukubali matokeo siku ya leo,hata hivyo mgombe wa CUFamejikuta anaangukia pua mbali ya kuwa mgombea bora kwa sera za kueleweka vituo kibao amepata maziro yakumwaga.
     Mgombea kupitia  Chama cha Mapinduzi   CCM Dokta Dalaly Kafumu  ameshinda uchaguzi wa  ubunge  katika jimbo la Igunga mkoani Tabora.

     Msimamizi wa uchaguzi   Protase Magayane     akitangaza  matokeo hayo amesema.

Kuwa  Dokta Kafumu amepata kura elfu 26434 dhidi ya mpinzani  wake  Joseph Kashindye wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema  aliyepata kura elfu 23 260.

     Amesema  kura zilizopigwa zilikuwa ni elf 53 672  ambapo kura halali ni  elfu 52 487  na zilizoharibika ni  kura elfu 1185.

     Aidha  msimamizi huyo amesema kuwa  jumla ya wapiga kura waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni laki   17077.


 MANENO OSWAD ADUNDWA NA KASEBA
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Iddy Azani akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa PST bondia Japhet Kaseba baada ya kumtwanga Maneno Oswald kwa Point jijini Dar es salaam jana.

MAONYESHO YA LONDON MODEL NETWORK YAFANA

 
 Mdau akipiga picha katika moja ya sanamu za Show hiyo ya London Model Network show iliyofanyika jijini London mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa  AURA uliopo MAYFAIR  ikiwashirikisha warembo kutoka pande zote za Dunia, Make up Artist, Stylist, na Designers

No comments:

Post a Comment