Pages

Pages

Thursday, November 10, 2011

BREAKING NEWS: TFF KWAWAKA MOTO....VIONGOZI WA VILABU WAGOMA


   Masaa machache baada ya Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Leodgar Tenga kuomba kukutana na viongozi wakuu wa vilabu 14 vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara kwa ajili kuzungumzia utata wa namna ya uendeshaji wa ligi kuu ya msimu ujao utakavyokuwa, sasa taarifa za muda huu zilizothibitishwa zinasema viongozi hao wa vilabu wamekutana jioni katika hoteli ya Movenpick na kuamua kuwa hawatokwenda kukutana na Tenga kesho kama alivyoomba.
  Viongozi hao wa vilabu wamesema sababu kuu ya kukataa kwenda kufanya mazungumzo na Tenga ni kwa sababu hawadhani kwamba kuna jipya lolote wataloambiwa ili kuweza kubadili msimamo wao wa ligi ya msimu ujao kuendeshwa na kampuni ya vilabu.
 “Hatuoni kama kuna umuhimu wowote wa kufanya majadiliano juu ya suala hili, sisi sote tumeshaamua kwamba msimu ujao ligi itaendeshwa na kampuni ya vilabu vishiriki, TFF na Tenga wenyewe hawataki, wanataka kamati itakayoteuliwa na Tenga ndio iendeshe ligi. 
  Tenga anataka tukae tujadili ajenda ipi? Sisi kwa pamoja tumeshaamua kwamba ligi ya msimu ujao itaendeshwa na kampuni yetu na huu uamuzi wetu wa mwisho,” alizungumza Geoffrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati maalum ya kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa Kampuni ya kusimamia ligi kuu kuanzia msimu ujao.


TONY BRAXTON AFUNGUKA DHIDI YA KASHFA YA KUTEMBEA NA KIJANA WA MIAKA 12
Yesterday, Toni Braxton and her sisters along with their mother made an appearance on The Wendy Williams show to promote the second season of “The Braxton Family Values.” There was a whole lot of Braxton personality on that stage as the sisters talked about Trina’s drinking problems, Tamar’s lighter skin, Towanda’s open relationship with her husband and Mama Braxton wanting to smack the p*ss out of Tamar. Toni also discussed her health, bankruptcy and money issues as well as her personal life. When she was asked if the rumors were true that she dated Terrence J from 106 and Park, Toni gave a pretty blunt answer:

You know that’s not true. I think he’s a cutie but he’s young; he’s 12. He doesn’t have no money. Sorry

I guess you better show some bank statements and come correct if you’re thinking about stepping to Toni B. She has major bills that need to be paid. She also revealed on the show that she’s been playing ‘in the snow’… if you catch my drift.

MTOTO WA BAKHERSA APIGA WAANDISHI  WA HABARI DAR

Jamal Bakhresa akitumia helmeti kuwapiga nayo waandishi wa habari waliodaiwa kumpiga picha yeye na mwendesha pikipiki mwenzake walipogongana katika Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana. Anayejaribu kumzuia ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda ambaye alipigwa na helmeti hiyo kichwani. Pembeni ni Cathbert Kajuna ambaye ni mwandishi wa gazeti la Kitangoma linalomilikiwa na Clouds Media ya jijini Dar es Salaam alikuwa akijaribu kumuamulia ugomvi.
Jamal kwa kitendo chake cha kuwaingilia wakati wakiwa kazini. Vitendo kama hivi vya kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao vimekuwa vikitokea mara wa mara ambapo vimekuwa vikiwasababishia hasara ya mali zao na vifaa kupoteza vifaa vya kazi.


 UTURUKI YAPATA WAZIRI MKUU MPYA
Papademos
Papademos kupambana na janga la madeni
Makamu wa zamani wa rais wa benki ya Ulaya Lucas Papademos ametangazwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ugiriki, kufuatia siku kadhaa za majadiliano.
Taarifa ya kuthibitishwa kwa nafasi ya Bw Papademos imetoka katika ofisi ya rais wa Ugiriki.

Viongozi wa vyama vikuu vitatu vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa wamekuwa wakikutana na rais waUgiriki kujaribu kufikia makubaliano.
Waandishi wa habari wanasema Wagiriki watakuwa na imani kuwa taarifa hizi zitaleta utengamano kuwasiadia kukabiliana na janga la madeni.
Bw papademos atahitaji kuongoza serikali ya mpito inayoundwa, kuhakikisha nchi hiyo yenye deni kubwa inapata fedha za kuisaidia, na kuidhinisha fungu la dharura la dola bilioni 177 la kimataifa kutoka katika nchi wanachama wanaotumia sarafu ya Euro pamoja na Shirika la Fedha Duniani IMF.
"Rais, baada ya mapendekezo kutoka kwa viongozi wa kisiasa waliohudhuria mkutano, wamemtaka Lucas Papademos kuunda serikali mpya," taarifa ya ofisi ya rais imesema, baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa kisiasa na Bw Papademos.
Serikali mpya itaapishwa adhuhuri ya Ijumaa, amesema afisa mmoja wa ofisi ya rais.
Bw Papademos atachukua nafasi ya waziri mkuu anayeondoka George Papandreu ambaye alitangaza kuwa anajiuzulu baada ya kutaka kuitisha kura ya maoni kuhusu fungu la kusaidia deni kutoka eneo la euro.
Waziri mkuu mpya atapigiwa kura ya kuwa na imani naye bungeni, siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa kituo cha TV cha serikali.
Soko la hisa la Ugiriki lilipanda ghafla baada ya Bw Papademos kuwasili katika ikulu ya rais kuijunga na majadiliano siku ya Alhamisi asubuhi.

No comments:

Post a Comment