Pages

Pages

Monday, November 14, 2011

MWANA FA KIDOLE JUU KAMA BI KIDUDE

Msaii wa hip-hop anafahamika zaidi kama Mwana FA, sasa ameamua kuandika mashairi yaliyotokana na wimbo wa taarab ambao uliimbwa na wasanii wakongwe wa muziki huo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
  Staa huyo ambaye sasa anatamba na video ya Unanijua Unanisikia ameamua kumshirikisha msanii Linah kutoka THT ambaye naye kwa upande wake amesimama vilivyo katika nafasi hiyo.
Mwana FA alisema kuwa wimbo huo unafanana kabisa na zile nyimbo walizoimba wasanii wakongwe wa taarabu hapa nchini aliowataja kwa majina ya Siti Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude. 
Wimbo huu kwenye chorus ameimba Linah na kurudia kwa melodi ile ile na kisha Mwana FA akaunganisha katika mashairi ya nyimbo hizo. Gitaa limepigwa na mmoja wa walimu wa muziki THT Cadinal Gento na biti ameisimamia Marco Chali kutoka MJ Records.


 

Ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akimfunza Marlaw namna ya kucheza kiduku jukwaani wakati msanii huyo alipotumbiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM la mtaa wa Pamba House,Dar es Salaam. 


LOWASSA:UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA NI BOMU LINATAKA KUILIPUA TANZANIA Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akipeana mkono na baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasichana Loreto mara baada ya kupokea mchango wa shule hiyo kwa ujenzi wa wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato jijini Mwanza.
Lowasa ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato kabla ya kuanzisha harambee maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2006 unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 12 ya vijana hawana ajira na wengi wa vijana hao wako mijini, asilimia 15 ya vijana nchini kati ya milioni 25 za vijana ndio wenye ajira, ilihali asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 -34 ni kundi kubwa ambalo ni tegemezi na halina ajira na hii ni kati ya nguvu kazi ya vijana milioni mbili na nusu ambao wako mijini na hawana ajira.
Amefafanua kuwa wakati hali hiyo ikitokea vijana 850,000 ambao wamekuwa wakihitimu elimu ya msingi, sekondari na vyuo wakiwa tayari kuingia kwenye soko la ajira lakini inasikitisha kati ya hao, ni asilimi 5 tu ndio wanaopata ajira ya kudumu, huku asilimia 35 ikijikita katika kilimo ambacho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo zile za uhaba wa pembejeo.

No comments:

Post a Comment