Pages

Pages

Sunday, November 13, 2011

TAIFA STARS WAINGIA KWA MBWEMBWE JIJINI DAR

 Wchezaji wa timu ya Taifa "TAIFA STARZ" wakiwasili kwa ndege toka nchini Chad ambako walifanikiwa kuicha timu ya taifa ya Chad bao2-1.
           
Kocha wa Timu ya TAIFA Jan Paulsen akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere leo jiji Dar baada ya kuwasili toka D'jamena,timu hizi mbili zitarudia hapo kesho nchini Tanzania kwa awamu ya mrudiano.


 CHALE 21 ZA DIAMOND NDIZO ZINAZOMSAIDIA KUWIKA ZAID?
 CHALE 21 alizochanjwa mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ zimewapa mshtuko watu wake wa karibu na kuanza kuzitafsiri katika matumizi mbalimbali.
  Chanzo kikaanika kweupe kuwa chale hizo ndizo zinazomsaidia msanii huyo kung’ara kwa kila wimbo anaoutunga na kuupeleka kwa mashabiki wake na pia kuwa na mvuto kwa mademu ambapo wanamshobokea............
  “Unajua wenzake wanasema zile chale zinamsadia jamaa kwenye nyimbo zake kuwa bora, lakini pia zinamfanya apendwe na mademu, we si unaona mwenyewe?”
  Diamond ameshadaiwa kuwa na uhuasiano wa kimapenzi na mastaa na wasio mastaa watano Bongo ambapo amewahi kukiri na kukataa.
Mastaa hao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2008), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus), Natasha (msanii wa nyimbo za Bongo Fleva) na sasa Wema Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006 ambaye amevishwa pete ya uchumba miezi miwili iliyopita.
   Diamond: Si kweli bwana, chale kweli ninazo ila sababu siyo eti nyimbo zangu zing’are au mademu wanishobokee.
   Diamond: Nilipokuwa mtoto niliwahi kusumbuliwa sana na ugonjwa wa kichomi cha mara kwa mara, ikafika wakati nikapelekwa kwa tabibu wa tiba asilia ndiyo nikachanjwa chale. Kwahiyo nimekua nazo.
  “Kama ni kuhusu nyimbo zangu kufanya vizuri, binadamu lazima waseme kila penye mafanikio. Kama kazi nzuri kwanini isikubalike. Pia mimi sishobokewi na mademu, nakutana nao kama wanavyokutana na wengine.


MBUNGE WA CCM AHUKUMIWA KIFUNGO.

Mh. Mbunge wa Mbarali Modestus Dickson mwenye kaunda suti katikati.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mbeya, imemtia hatiani Mbunge wa Mbarali, Modestus Dickson Kilufi kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno kwa kukusudia na kumuhukumu kwenda Jela miezi 10 au kulipa faini ya shilingi 500,000.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa hukumu hiyo ilitolewa leo na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Michael Mtaite ambaye alikuwa akisikiliza shauri hilo, ambalo Kilufi alishtakiwa alidaiwa kutishia kwa maneno kumuua Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruwiwa wilayani Mbarali, Jordan Masweve.

No comments:

Post a Comment