Pages

Pages

Sunday, December 18, 2011

BREAKING NEWS: MR.BLUE AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI


                                         Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Msanii wa bongo flava Mr.Blue amefiwa na mama yake mzazi,chanzo cha habari hakikufanunua vema kutokana na tatizo la mawasiliano ila punde tutawajuza habari kamili hivi punde.


MWANAMKE ALIEVUNJA NDOA YA KOBE BRYANT HUYU HAPA

Oh Kobe, when will you learn? Please excuse the NBA player if his game is a little off this season, he has a lot on his plate. 

Yesterday the news hit the web that Kobe and his wife of 10 and a half years had filed for divorce stating irreconcilable difference. Vanessa Bryant was no stranger to the allegations that her baller husband was cheating with other women, but sources claim the straw that broke the Laker's marriage was his affair with Playboy Model Jessca Burciaga.


Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”
Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki, Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.


Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro yote inayoendelea ndani ya chama.
“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu. Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yoyote inayopenda amani,” alisema Mwasada.
Hata hivyo, Kafulila juzi alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.
“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu," alisema Kafulila na kuongeza.
“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”
Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.


WADAU WA MCHEZO WA NGUMI WASHIRIKI MAZISHI YA BONDIA MOHAMEDI KIDEVU LEO

Baadhi ya waombelezaji wakjisghikilia mwisli wa aliyekuwa bondia Mohamedi Kidevu kwa ajili ya kwenda kuzika maeneo cha Chanika leo mchana.

No comments:

Post a Comment