Pages

Pages

Tuesday, December 6, 2011

BREAKING NEWS: NDANDAA COSOVO ATIMULIWA NCHINI TANZANIA

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya dansi aliyepata kujizolea sika kem kem nchini wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica, Ndanda Cosovo ‘Kichaa’ amekamatwa masaa machache jijini Arusha pamoja na wanamuziki wa bendi yake mpya.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto kwa njia ya simu, Ndanda Cosovo, alisema kuwa amekamatwa yeye pamoja na wanamuziki wake wote na kuwekwa chini ya ulinzi ambapo kwa sasa wanasubiri kupelekwa Rumande hadi kesho watakaposafirishwa kurudi kwao Kongo.
Aidha Ndada alisema kuwa ameshangazwa na uongozi wa Uhamiaji kukagua vibali vyake vya kuishi nchini na kumwambia kuwa vibali hivyo ni ‘Feki’ hali ya kuwa alikata na kulipia vibali hivyo jijini Dar es Salaam.
“Mimi nashangaa sana kama Mkurugenzi wa Uhamiaji anaweza kupokea pesa na kisha akatoa vibari Feki, hii si sawa kwani mimi nilikuwa nikiishi Tanzania kwa uhalali na kufuata taratibu zote na ndiyo maana nikawa nikifanya kazi zangu bila kificho, leo nakamatwa nakuambiwa vibari vyangu ni feki kwa kweli nimesikitika sana,
Napenda kuwaageni marafiki zangu wote mbaki salama kwani tuliishi kwa amani na kusaidiana kama ndugu leo hii naambiwa nimevunja sheria mbona hawajaniambia hivyo tangu nilipokuwa nikiwalipa pesa za vibari??” alimaliza kwa kuhoji Cosovo.

KILIMANJARO STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CUP


Timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuingia nusu fainali ya CECAFA Senior Challenge Cup 2011, baada ya kuifunga timu ya Malawi kwa goli moja kwa bila. Goli la Stars lilifungwa na kiungo Nurdin Bakary katika kipindi cha kwanza na kudumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kwa matokeo hayo Kili stars sasa itacheza na Uganda katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Alhamisi.

No comments:

Post a Comment