Pages

Pages

Thursday, December 15, 2011

SALHA ISRAEL AKABIDHIWA JEEP PATRIOT LEO

  Miss Tanzania Salha Isarel akipokea funguo ya gari aina ya Jeep Patriot kutoka kwa Meneja Matukio na Udhamini wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa shindano hilo la Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw. Alfred Minja. Gari hiyo ina thamani ya shilingi 72 Milioni.
  Miss Tanzania Salha Isarel akionyesha funguo ya gari aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi milioni 72mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Udhamni na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa wa pili toka kulia kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw. Alfred Minja.
Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akifungua mlango wa gari lake aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi 72 milioni tayari kwa kuondoka nalo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa hayupo pichani,Ikiwa ni zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.

 DKT.KIKWETE AKIWA NA DR. MIGIRO NA BALOZI MULAMULA KAMPALA 

Rais Jakaya Kikwete akimpongenza Balozi Liberata Mulamula kwa kazi nzuri aliyoifanya katika sekreteriati ya Maziwa Makuu kwa miaka mitano. Pembeni ni Dr Asha-Rose Migiro Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Rais Kikwete na Dr Migiro na Balozi Mulamula leo leo December 15, 2011 katika hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongoji cha Munyonyo nje kidogo ya jiji la Kampala kunakofanyika mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) ambapo Balozi Mulamula ndiyo amemaliza rasmi muda wake wa kufanya kazi kama Katibu Mtendaji wa (ICGLR) na kumuachia kiti Prof. Lumu Alphonse Ntumba Luaba (59) wa DRC.

No comments:

Post a Comment