Pages

Pages

Tuesday, January 3, 2012

AKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA SHUGHULI ZA MAZIKO 'DUA' YA MAREHEMU BALOZI ATHUMAN MHINA

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazazi wa CCM Zanzibar, Bi. Dogo Mabruk, wakati alipokuwa akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, marehemu Balozi Athuman Mhina, kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za maziko, Madale jijini Dar es Salaam, leo Januari 3, 2012. Kulia ni Sophia Simba. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, marehemu Balozi Athuman Mhina, kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za maziko, Madale jijini Dar es Salaam, leo Januari 3, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment