Pages

Pages

Monday, January 2, 2012

EXCLUSIVE:JACKY PENTEZEL APIGWA KIBUTI NA TIMBULO...PENZI LAO VIPANDEVIPANDE!!

 EXCLUSIVE DETAIL: Habari za uhakika zilizotufika hivi punde ni kwamba Jacky Pentezel amemwagwa kimapenzi na msanii wa bongo flava Timbulo,penzi lao lililoonyesha wivu na huba UNIQUEENTERTZ imebaini.
  Mnyetishaji wa habari hizi amesema kuwa Timbulo kampa kibuti Jacque kutokana kumchoka kimapenzi muigizaji huyo na radha ya mapenzi haipo tena kati ya wawili hao.
    Awali Jacque alionekana kulewa zaidi na penzi la kijana huyo mbana pua ambae anatamba na vibao viwili vinavyosumbua katika vituo mbalimbali vya habari.
  Kubwa zaidi ni kwamba inasemekana Timbulo amepata demu mwingine wa kishua zaidi ambae anamaliza shida ndogondogo za kijana huyo hivyo kumpelekea kumpa kisogo Jacque,stay tuned dont touch your keyboard ntaongea na jacque then ntakujuza binti huyo anajisikiaje kumwagwa na chekibob huyo.

No comments:

Post a Comment