Pages

Pages

Monday, January 30, 2012

JOKATE AMPAKA WEMA KIJANJA

   MSANII aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo, amesema kuwa fani hiyo ya urembo imekuwa kama kimbilio la wanawake wahuni kitu ambacho kinachangia kuifanya ikose heshima yake kama ilivyokuwa zamani.

Mrembo huyo mwenye heshima katika fani hiyo, alisema kuwa endapo kutakuwa na sheria ambayo inambana miss yoyote ambaye anaokekana kwenda kinyume basi wanawake ambao wangependa kushiriki fani wangekuwa ni wale wenye tabia njema pekee.


Alisema kuwa wapo wengine ambao wanatabia nzuri lakini baada ya kushiriki katika fani hiyo wanabadilika na kufuata tabia za watu wahuni huku wakizani ni nzuri wakati ndiyo wanapoteza sifa zao kama warembo.


Alisema fani hiyo ni kazi kama nyingine hivyo kunapotokea mtu mwingine anaivunjia heshima anasababisha hata warembo wengine waliotamani kushiriki kukata tamaa kwa kuhisi endapo na yeye akishiriki anaweza kuwa na tabia za mtu fulani.


“Unajua hakuna kitu kibaya kama kuichafua kazi ambayo imekutoa kwa sababu kuna mtu mwingine anakuwa anatamani kushiriki fani hiyo, lakini kutokana na tabia aliyonayo mtu fulani ambayo si nzuri basi inakuwa inakatisha tamaa na wengine kushiriki,”
Alisema.

No comments:

Post a Comment