Pages

Pages

Monday, January 30, 2012

WATU 40 WAULIWA NA WEZI WA MIFUGO SUDAN


Wafugaji Sudan Kusini
Kambi za wafugaji Sudan Kusini
Maafisa wa serikali katika Sudan Kusini wanasema watu wasiopungua 40 wameuwawa na kundi la watu wenye silaha waliokwenda kuiba mifugo.
Baadhi ya taarifa zinasema idadi ya watu waliouwawa ni zaidi ya 100 kwenye uvamizi, huo uliotokea kwenye kambi moja katika jimbo la Warrap.
Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Kusini ameilaumu serikali ya Sudan kwa kuwapa silaha washambuliaji hao, ambao ni kundi la wapiganaji kutoka jimbo jirani la Unity.
Mvutano umeendelea kuwepo tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka Sudan mwezi Julai, kufuatia vita vilivyochukua miaka mingi.
Afisa ammoja katika jimbo la Warrap ameambia gazeti la Sudan Tribune linaloandikiwa mjini Paris kwamba vijiji vinavyokaliwa na watu wa jamii ya Luac Jang katika wilaya ya Tong mashariki walishambuliwa Jumamosi alfajiri.
Spika wa bunge Madot Dut Deng amesema ameambiwa na maafisa kwamba zaidi ya watu 76 wameuwawa, na wengine hajulikani walipo.
Afisa mwingine katika jimbo hilo aliambia gazeti hilo watu katika eneo lililoshambuliwa wanasema waliouwawa ni zaidi ya 100.
Waziri wa mambo ya ndani Alison Manani Magaya amesema mashambulizi hayo yaliendeshwa na kundi la wapiganaji kutoka jimbo jirani la Unity.
"kundi hili lilipewa silaha na serikali ya Khartoum," aliambia gazeti la AFP, lakini hakutaja ni kundi gani.
Sudan Kusini ilipata Uhuru tarehe 9 Julai mwaka 2011 kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe na Sudan.
Tatizo lililochangia mzozo hadi sasa ni kwamba silaha nyingi zimezagaa.
Silaha hizo zinatumika katika mapigano ya kikabila, ambayo mara nyingi yanahusu mifugo kutokana na umuhimu wake miongoni mwa jamii nyingi katika Sudan Kusini.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon siku ya Jumapili alitoa wito kwa viongozi wa Sudan na Sudan Kusini kufanya makubaliano kuhusu namna ya kugawana utajiri unaotokana na mafuta, ambayo husababisha mvutano baina ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment