Pages

Pages

Saturday, January 28, 2012

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA JESHI LA POLISI NA MKUU WA MKOA WA TANGA

viongozi wa Serikali na wananchi wa kijiji cha Nduu,Mombo mkoani Tanga wakitafuta namna ya kuwatoa askari wa kikiso cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Tanga mara baada ya gari lao lenye namba za usajiri PT 2000 aina ya Toyota Landcrusser kuacha njia na kupinduka bondeni wakati wakiwa kwenye ziara ya Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal iliyotokea jana eneo la Nduu Mombo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerari Said Mwema na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa, kufuatia ajali ya gari la Polisi lililopata ajali na kusababisha kifo cha askari sambamba na kujeruhi wengine, ajali iliyotokea jana katika barabara itokayo Lushoto kuingia mji mdogo wa Mombo, gari ambalo lilikuwa mwishoni mwa msafara wa Makamu wa Rais uliokuwa ukitokea wilayani Lushoto.
Makamu wa Rais alikuwa akimalizia ziara yake mkoani Tanga, ziara aliyoianza Januari 24 na kuikamilisha jana Januari 27 wilayani Lushoto. Msafara wa Makamu wa Rais ulikuwa unatoka Lushoto ukielekea Hale, ambako huko Makamu wa Rais amefika salama. Makamu wa Rais amesikitishwa sana na tukio hilo na amewapa pole Mkuu wa Jeshi sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, na anabainisha kuwa tukio hilo limemgusa sana na anawatakia moyo wa ujasiri na uvumilivu kufuatia tukio hili ambalo limekuja katika kipindi ambacho hakikutarajiwa.
Makamu wa Rais anatarajiwa kuondoka mjini Tanga kesho kufuatia kuhitajika kusimamia mkutano wa Kamati ya Muungano unaofanyika kesho asubuhi jijini Dar es Salaam, sambamba na kusimamia majukumu mengine ya serikali kufuatia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa nje ya nchi kikazi kwa sasa.“Naamini mkoa wa Tanga na Jeshi la Polisi watatoa huduma zote zinazohitajika kwa wafiwa sambamba na majeruhi, nami binafsi nitafatilia kwa ukaribu,” anasema Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

No comments:

Post a Comment