Pages

Pages

Saturday, January 28, 2012

MSD YATOA MSAADA WA SH.MIL.10 KWA TWIGA STARS

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu hiyo inapambana na Namibia kesho katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.
Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Kutoka kulia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo
Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto) akitoa shukurani kwa MSD kuipatia timu hiyo msaada. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah wakiwa na furaha wakati wa hafla ya MSD, kukabidhi msaada wa Sh. Mil. 10 kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia.
Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia (kushoto), akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka kwa wanawake. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah

No comments:

Post a Comment