Pages

Pages

Tuesday, January 10, 2012

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MWENGE JIJINI DAR

 Baadhi ya raia wema walifika kutoa msaada.
Sehemu ya juu ya nyumba hiyo iliyoteketea.
Mmoja wa askari wa Zimamoto akipambana na moto huo.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa.
Pendo Julius, jirani na mmoja wa mashuhuda wa moto huo akizungumza na vyombo vya habari.
Zimamoto wakipambana na moto huo.
Moja ya magari ya Zimamoto.
MOTO umeibuka asubuhi ya leo katika nyumba iliyopo maeneo Mwenge, jijini Dar es Salaam, jirani na ofisi za Radio Sibuka FM na kuteketeza sehemu kubwa ya jengo hilo na baadhi ya mali zilizokuwemo ndani yake.
Chanzo halisi cha moto huo hakikuweza kufahamika mara moja ingawa inadaiwa kuwa huenda ilikuwa ni shoti ya umeme ambayo ilichangiwa na mitungi ya gesi iliyokuwepo katika nyumba hiyo. Hakuna mtu yeyote aliyedhurika na moto huo.

No comments:

Post a Comment