Pages

Pages

Monday, January 16, 2012

SIMBA NA TUSKER YA KENYA ZATOKA SARE 1-1

Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na Tusker ya Kenya wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mpambano wao wa kirafiki, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. ambapo timu hizo zimetoshana nguvu baada ya Simba kupata goli kwa njia ya penati lililofungwa na mchezaji wao Patrick Mafisango katika kipindi cha kwanza. Katika kipindi cha pili Tusker waliswawazisha goli kupitia mchezaji wao Patrick Kagogo na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa suluhu ya magoli 1-1 mpaka mpira unamalizika, huku mchezo wa leo ukiwa mzuri kwa upande wa timu zote, japokuwa Tusker ya Kenya ndiyo iliyoenda mara nyingi katika lango la timu ya Simba ya Tanzania. Tofauti na mchezo wa jana katika mchezo wa timu za Yanga na Sofapaka ya kenya kwenye uwanja huohuo wa Taifa, ambapo mpira ulionekana kuwa wa upande mmoja na usio na upinzani wakati Yanga ilipoifunga timu hiyo magoli 2-1 huku Sofapaka ikionyesha kiwango cha chini sana tofauti na ilivyozoeleka.

No comments:

Post a Comment