Pages

Pages

Friday, January 20, 2012

ZEE LA NYETI LAFIKISHWA KORTINI MBEYA

 Baba mzazi wa binti aliyebakwa na Mzee Asangile Kihaka (70), anayefahamika kwa jina la Bwana Ekson Nazareth  (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini.. 
 Mmoja wa wananchi wa eneo la Ghana akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, amba ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mzee Asangile Kihaka mwenye umri wa miaka 75 mkazi Ghana amefikishwa katika mahakamani ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya jana akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12 disemba 14 mwaka jana.

Akisoma shtaka linalomkabili mzee huyo mwanasheria wa Serikali Roda Ngole mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zabibu Mpangule amesema mzee Asangile alitenda kosa hilo akiwa nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kumpelekea kuni nyumbani kwake na baada ya mtoto kufika ndani mzee huyo alianza kumwingilia kimwili kwa nguvu.

Amesema kitendo hicho ni kinyume cha kifungo cha Sheria 130 sura ya pili E na kifungu namba 131 sehemu ya kwanza sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zainabu Mpangule ameihairisha kesi hiyo hadi February mosi mwaka huu na kwamba mtuhumiwa amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana ya shilingi laki tano.

No comments:

Post a Comment