Pages

Pages

Friday, January 20, 2012

JK KATIKA MSIBA WA MAREHEMU JEREMIAH SUMARY JIJINI DAR ES SALAAM

Jakaya Kikwete Akimpa pole mjane wa Marehemu Jeremia Sumary, Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha wa wa zamani aliyefariki leo asubuhi jijini Dar es salaam. Hapa ni nyumbani kwa marehemu, Mbezi Beach, Dar es salaam jioni hii.Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo.Jakaya Kikwete akiongea na ndugu wa marehemu pamoja na Spika Anne Makinda na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ambaye ni mzazi wa binti aliyeolewa na mtoto wa marehemu Sumary.Rais Jakaya Kikwete akitoa pole kwa wafiwa.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment