Pages

Pages

Saturday, February 4, 2012

CHRISTINA SHUSHO, MARTHA MWAIPAJA WANUSURIKA KICHAPO

                           Christina Shusho


 Martha Mwaipaja
MASTAA wa nyimbo za Injili nchini, Christina Shusho na Martha Mwaipaja (pichani) hivi karibuni walinusurika kula kichapo kama wasingekimbilia sehemu na kujificha.
Aibu hiyo ilitokea kwenye uzinduzi wa albamu ya mwanakwaya mwenzao, Elizabeth Ngaiza iitwayo Enendeni Kwa Roho uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kilimanjaro, Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar.
Kwa mujibu wa macho ya mapaparazi wetu, wakati shughuli ya uzinduzi ikiendelea, alitokea mwanaume mmoja akiwa na watoto wawili na kudai yeye ni mume wa Elizabeth na hajabariki uzinduzi huo kwa sababu alifichwa.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Jones alipanda jukwaani na kuchomoa nyaya za umeme zilizounganishwa kwa ajili ya muziki na hivyo kufanya eneo la tukio kuwa kimya kwa muda huku akipiga mateke spika.
Christina Shusho na Martha Mwaipaja ambao walikuwa wakimsindikiza Elizabeth, walipata upenyo kwa kujibanza sehemu ili kudumisha amani yao ambayo ilikuwa imetibuliwa na ‘mvamizi’ huyo.
Akizungumza na gazeti hili, Elizabeth alikiri kuwa jamaa huyo ni bwana’ke wa zamani na alifika eneo hilo kwa lengo la kuangusha varangati ili kuvuruga uzinduzi wake.
Kufuatia tukio hilo, Eliza aliwaomba radhi mashabiki wote waliohudhuria onesho hilo hasa wale walioumia na kuwaambia kuwa licha ya uzinduzi huo kuvurugwa lakini tayari albamu hiyo imeshaingia madukani.

No comments:

Post a Comment