DULLY SYKES.T.I.D WAZITOSA TUZO ZA KILI 2012
Mara
baada tu ya kutangazwa kuwa mmoja wa watakaoshiriki kupigiwa kura
kwenye hatua ya awali ya mchujo wa tuzo za BASATA KILIMANJARO MUSIC
AWARDS, msanii wa bongo fleva Dully Sykes amekuja juu na kulaumu
wahusika kwa kitendo chao cha kumuweka katika kinyang'anyiro hicho
wakati alishasema hataki siku nyingiiii."Nilishawaambia sitaki kuwepo
tena katika tuzo zao, tangu mwaka juzi, lakini nashangaa kuona
wanaendelea kuniweka tu, kwani wananiona mimi ndio msanii pekee, wakati
ule wa hits kama nyambizi, Hi na zinginezo mbona hawakunipa tuzo? au
walidhani mi ni msanii ambae ningeishia kati tu, lakini baada ya kuona
nipo na naendelea kuwepo ndio wanajifanya kunitambua..nimesema
sitaki.Hata hivyo baada ya BASATA kuulizwa kuhusu tuhuma hizo walisema
msanii kama hataki kuwemo kwenye tuzo hizo basi aandike barua BASATA ya
kujitoa lakini sio kwa maneno tu.
No comments:
Post a Comment