Pages

Pages

Friday, February 10, 2012

HATIMAYE WAZIRI MKUU AWAFUKUZA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA MGANGA MKUU WA SERIKALI, BAADA YA KIKAO NA MADAKTARI WALIOGOMA KWA WIKI KADHAA.

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza leo na Madaktari kufuatia sakata la mgomo wao uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa wakati alipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kukutana nao na kusikiliza malalamiko yao.Pia kutokana Malalamiko ya Madaktari hao ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo Mtasiwa.Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda amesema amewafuta kazi wakuu hao kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa taifa.Waziri Mkuu amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo awali. 
Mh. Waziri Mkuu akisikiliza kwa makini malalamiko na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na madaktari .
Baadhi ya Madaktari wa Muhimbili wakizungumza huku umati wa madaktari wengine ukiwa umetulia kusikiliza.
Madaktari wakishangilia wakati wenzao wakitoka mapendekezo mbali mbali kwa Waziri Mkuu.
Sehemu ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda wakati akizungumza nao leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hospitali hiyo leo.
Waziri Mkuu akiagana na baadhi ya Madaktari wa Muhimbili waliokuwa nje ya ukumbi wakati akiondoka.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick mara baada ya kuzungumza na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili .

No comments:

Post a Comment