Pages

Pages

Thursday, February 2, 2012

KAFULILA AILIPUA SERIKALI ASEMA WAPO WANAOLIPWA 20 ML KWA MWEZI

Mbunge  wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, ambaye yuko kwenye mzozo na chama chake kilichomfukuza uanachama, alisema kinachosumbua kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wenye usawa wa ulipaji mishahara na posho ndani ya serikali. Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi. “Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000,” alisema na kuhoji hapa haki iko wapi. Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.

No comments:

Post a Comment