Pages

Pages

Friday, February 10, 2012

MADAKTARI NA WAUGUZI WAREJEA KAZINI HOSPITALI YA TAIFA NA AMANA ILALA.

Afisa Uhusiano katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Aminieli Eligaesha akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu kurejea kwa huduma za afya katika hospitali hiyo, kufuatia mgomo wa madaktari bingwa nawauguzi uliofanywa katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akipitia jalada kabla ya kwenda kutoa matibabu kwa mgonjwa katika wodi ya Kibasila ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.
Daktari Charles Some wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimtoa damu kwa ajili ya vipimo vya matibabu kwa Bi. Upendo Msangi katika wodi ya kibasila. Madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo wamerejea kazini leo (jana) kufuatia agizo lililotolewa naWaziri Mkuu Mizengo Pinda jana (juzi) la kuwataka kurejea katika maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika hospitali ya amana, wakisubiri huduma za matibabu katika hosptali hiyo, kufuatia kurejea kazini kwa madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo mara baada yamgomo uliodumu katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi wa kubeba wagonjwa katika hospitali ya Amana Ilala, Mohamed Ally akimpeleka katika chumba wagonjwa, Bi Domitila Haule tayari kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo. Madaktari na wauguzi wamerejea kazini leo kufuatia mgomo waliouitisha takribani wiki tatu sasa.

No comments:

Post a Comment