Pages

Pages

Friday, February 3, 2012

SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA YAFANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akitoa neno lake la shukrani katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G.K. Rwakibarila na Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda hiyo.
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Kanali John Mzurikwao, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G. K. Rwakibarilla, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya, Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Sumbawanga Prosper Rwegerera wakiangalia Kwanya iliyokuwa ikitumbuiza katika Sherehe za Siku ya Sheria Nchini Leo.
Mhe. Jaji Mfawaidhi G. K. Rwakibarila akikagua Gwaride hilo.
Mhe. Jaji Mfawidhi akiteta jambo na wenzake mara baada ya kukagua Gwaride la heshma.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakijumuika kwenye kwaya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuika kupanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Sheria .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, katibu wake Frank Mateny (kushoto), Afisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George Kiria na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Rukwa wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakisubiri kuanza kusikiliza mashauri yaliyopangwa kusikilizwa katika mahakama hiyo yaliyombatana na maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini.

No comments:

Post a Comment