Pages

Pages

Friday, February 10, 2012

SINTA NA DIAMOND WAMENDEANA KIMYA KIMYA

    
Sintah na Diamond, wameanza silimulizi za mapenzi juu ya wapenzi wao wa zamani huku kukiwa na tetesi kuwa wanaweza kukifanya kitu hicho kuwa kweli katika maisha yao.

Sintah
ni mmoja kati ya wasanii wenye sura yenye mvuto ambapo anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na msanii huyo muziki wa kizazi kipya.

Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza
kwa sharti la kutotajwa jina lake, kilisema kuwa wasanii hao wamekuwa karibu tangu Diamond alipoachana na Wema Sepetu.

Kilisema kuwa kikubwa ambacho wasanii hao wamekuwa wakizungumza ni juu ya wapenzi wao wa zamani, ambapo wanaonekana kufarijiana huku wakipeana moyo namna ya kupata mpenzi mwema na aliyetulia.


“Sidhani kama kuna kitu chochote kibaya ambacho wanakifanya, lakini naamini wanachozungumza ni juu ya maisha ya mahusiano kwani wanaonekana kuzungumzia sana wapenzi wao wa zamani,”
kilisema chanzo hicho cha habari.

Chanzo hicho kilisema kuwa hata hivyo katika maongezi yao wanaonekana kuwa karibu zaidi kiasi kwamba wanaweza kuzua utata juu urafiki wao.


Hata hivyo
Sintah, alipotafuta kuzungumzia ishu hiyo, alisema yupo karibu na Diamond, lakini haimanisha kama wanaweza kuanzisha mahusiano kwani anachukulia kama mdogo wake.

Alisema kwa upande wake yupo karibu na kila mtu hivyo kuonekana na
Diamond, haimaanishi ni mpenzi wake au anataka kuanzisha mahusiano naye.

Naye
Diamond, alipoulizwa juu utata huu alisema kuwa hakuna kitu kinachoshindikana kwani Sintah ni mtu mzuri ambaye amekuwa akizungumza naye mambo mengi ya maisha.

No comments:

Post a Comment