Pages

Pages

Monday, February 13, 2012

ZAMBIA YANYAKUA UBINGWA WA AFRICA 2012

 Timu ya Zambia ikishangilia ushindi baada ya kutwaa Kombe la Mataifa Afrika jana.

ZAMBIA jana ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuichapa Ivory Coast kwa penalti 8-7 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Libreville, ambapo Stoppila Sunzu alifunga penalti ya mwisho ya ushindi.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na kuhudhuriwa na wanasoka wengi maarufu akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) Sepp Blatter, Pele wa Brazil na Samuel Eto’o, ulishuhudia timu hizo zikienda hadi dakika 120 baada ya kumaliza dakika 90 kwa suluhu.

Ivory Coast ambayo ilichezesha mastaa kibao akiwemo, mshambuliaji Didier Drogba, Solomon Kalou wanaocheza Chelsea pamoja na Gervinho wa Arsenal, ilishuhudia Drogba akikosa penalti katika dakika ya 69 baada ya Gervinho kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Ivory Coast ambayo ilifika fainali bila nyavu zake kutikiswa ilionyesha uhai wa hali ya juu dakika 15 za mwisho lakini safu ya ulinzi ya Zambia ilikuwa makini kuondoa hatari.

Hata hivyo, Zambia ambayo ilikuwa ikicheza kandanda la kasi na kushangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki waliokuwa wamejazana uwanjani itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi.

Huu ni ubingwa wa kwanza kwa Zambia katika michuano hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1957.

No comments:

Post a Comment