Pages

Pages

Sunday, March 4, 2012

BABY MADAHA ATI,ULIWA NYUMBANI NA WAZAZI WAKE,NI BAADA YA KUKATAA KUOLEWA NA KIBOPA


  BAADA ya sakata lililokuwa linamkabili Baby Madaha, kutoka kwa wazazi wake la kutakiwa kuolewa mapema iwezekanavyo, limechukua ukarasa tata ambapo sasa amefukuzwa kwao kwa kile kinachodaiwa ni kukaidi suala hilo.
  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huku akitokwa na machozi, msanii huyo alisema kuwa hayupo tayari kufanya wanavyotaka na uamuzi waliuchukua baada kikoa cha familia ni kumfukuza nyumbani.
  Alidai kuwa njia waliyoitumia haiwezi kuwa shinikizo kwake kwani ataenda kutafuta nyumba ya kupaga na ataishi maisha yake kama kawaida.
  “Hivi karibuni walikaa kikao na lengo kubwa lilikuwa ni kunijandili kuhusu ishu yao ya kutaka mimi niolewe lakini kwa upande wangu siwezi kufanya kitu wanachokitaka wao wakati kwa sababu roho yangu bado hajaipenda,”
alisema.
  Hata hivyo mmoja ya wanafamilia aliyezungumza na 
mandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotajwa jina lake, alisema kuwa ni kweli wazazi wao walitaka afunge ndoa lakini amekataa kutimiza suala hilo, kitu ambacho kimewaudhi wazazi na kuamua kuchukua maamuzi hayo mazito.

No comments:

Post a Comment