Pages

Pages

Sunday, March 4, 2012

TWANGA PEPETA YAZIDI KUSAMBARATIKA LILIAN INTERNET ATIMKIA MASHUJAA MUSICA

Lilian Tungaraza (Intanet)
BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imezidi kuisambaratisha bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ baada ya kumyakua mnenguaji wake mahiri,Lilian Tungaraza maarufu kama ‘Intanet’.
Meneja wa Mashujaa Band Maximilian Luhanga alisema kwamba wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika idara hizo na tayari wameshasaini mkataba wa kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili ambao onyesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika jumatano ijayo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Hii ni mara ya pili kwa Mashujaa kuchukua mwanamuziki kutoka Twanga Pepeta, ambapo mapema mwaka huu ilimyakua mmmoja ya waimbaji mahiri, Charlz Gabriel ‘Chaz Baba’

No comments:

Post a Comment